Wednesday, August 12, 2020

SERIKALI YAWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WADOGO KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA


Naibu waziri wa Biashara na Viwanda , Mhe. Stella Manyanya akimsikiliza Mmiliki wa kiwanda cha Afya Sembe Bw.David Kihwele  wakati wa ziara yake ya ufutiliaji kupitia sido jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Biashara na Viwanda , Mhe. Stella Manyanya akitoa maelekezo kwa  Mmiliki wa kiwanda cha Afya Sembe Bw.David Kihwele  wakati wa ziara yake ya ufutiliaji kupitia SIDO jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Biashara na Viwanda , Mhe. Stella Manyanya akimsikiliza Meneja wa SIDO Kanda ya Kati Sempeho Manongi  wakati wa ziara yake ya ufutiliaji kupitia sido jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Biashara na Viwanda , Mhe. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza ya kufutilia wazalishaji wadogo kupitia SIDO jijini Dodoma.

Meneja wa SIDO Kanda ya Kati Sempeho Manongi akitoa tathimini ya ziara ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya ufatiliaji wa wazalishaji wadogo wadogo kupitia SIDO  jijini Dodoma.

………………………………………………………………………..

Na. Alex Sonna, Dodoma
Serikali imesema kuwa katika kuwawezesha wamiliki wa viwanda vidogo itahakikisha inapambana kukuza kundi la kati ambalo linatakiwa kuwa na uzalishaji wenye kiwango bora na

kuleta ajira nyingi kwa watanzania.

Kauli hiyo imebainishwa na Naibu waziri wa Biashara na Viwanda , Mhandisi Stella Manyanya wakati wa ziara yake ya ufutiliaji wazalishaji wadogo wadogo kupitia sido baada ya kuona wazalishaji wengi wanakosa maeneo mazuri ya kufanyia kazi hususani katika maswala ya viwanda.

“Mfanya biashara anatakiwa ajenge kwanza jengo halafu anunue mitambo kisha aanze kuzalisha jambo ambalo lililofanya wengi kushindwa kuzalisha kwa kiwango kikubwa”, ameeleza Mhe. Manyanya.
Aidha amesema kuwa kwa sasa unakta viwanda vidogo vidogo ni vingi sana ukilinganisha na viwanda vya kati.
Hivyo wizara inahakikisha inapambana kuhakikisha inainua na kulinda kundi la viwanda vya kati ili kuongeza tija katika uzalishaji na ongezeko la ajira nchini.
“Wizara imeamua kujenga mabanda ambayo yanawezesha wenye viwanda kuleta mitambo yao na kufanya kazi na kendelea kutoa elimu juu ya uzalishaji kwa ubora stahiki kutoka sido”,ameeleza Mhe. Manyanya.

Katika hatua nyingine amesema kuwa majengo hayo yamekamilika na yote yamejaa wafanya biashara hata mwaka haujafika hii ni ishara tosha ya kuwa tukiwawezesha hawa tutaweza kulinda uchumi wetu na ubora wa bidhaa .

“Natoa wito kwa mikoa mingine waliopata kujenga mabanda haya kufanya uhamasishaji kama Dodoma na kuhakikisha yanaanza kufanya kazi ili wafanya biashara kufanya kazi zao katika mazingira sahihi na kupata ubora wa bidhaa”,amesisitiza Mhe. Manyanya

Meneja wa SIDO Kanda ya Kati Sempeho Manongi amesema wanajukumu la kutoa mafunzo na kuwawezesha kupata mikopo na kutumia teknolojia ili kufanikisha kazi zao za uzalishaji katika kazi zao.
Pia amesema kuwa viwanda hivyo vitaongeza tija katika kukuza ajira na kupunguza janga la ukosefu wa ajira nchini
Hivyo wajasiriamali wa Dodoma wajitokeze kuweza kupata mafunzo na kuhakikisha wanapata elimu itakayo wasaidia katika kuzalisha nafaka zenye bora katika viwanda vyao.

Kwa upande wake Mmiliki wa kiwanda cha Afya Sembe Bw.David Kihwele ametoa neno la Shukrani kwa kusma kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwawezesha mazingira sahihi ya kufanyia baisahara zao na kuwa bidhaa itakayozalishwa hapo itakuwa katika ubora unao hitajika katika masoko.

 

No comments :

Post a Comment