Serikali
imeendelea kuweka mikakati endelevu ya kuwawezesha vijana nchini
kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali ili kuendelea
uchumi wa Taifa.
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,
Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde alipokuwa akizungumza na waandishi
wa Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani “International
Youth Day” ambayo uadhimishwa kila Agosti 12 huku Mwaka huu 2020 kauli
mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni “Ushirikishwaji wa Vijana katika
Mstakabali wa Dunia”.
Naibu
Waziri Mavunde alieleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibari inayoongozwa na Rais wa Zanzibar ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein zimekuwa
zikichukua hatua mbalimbali za kuwashirikisha vijana katika nyanja
mbalimbali zenye lengo la kuendeleza nchi yetu.
“Serikali
yetu katika kutambua mchango wa vijana katika ujenzi wa Mataifa yao
inaunga mkono kauli mbiu iliyotolewa na Umoja wa Mataifa katika
kuadhimisha siku hii muhimu, hivyo itaendelea kuweka mifumo imara ya
kitaasisi na kisheria ambayo inawapa vijana fursa pana ya kushiriki na
kushirikishwa katika michakato yote ya maendeleo iyoyomo nchini,”
alieleza Mavunde
Alieleza
kuwa Serikali imeandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ambayo
imetamka wazi namna mifumo ya kisheria na kitaasisi iliyoweka katika
kuwezesha ushiriki wa vijana katika maendeleo ya Taifa, pia elimu bora
imekuwa ikitolewa kwa vijana lengo ikiwa ni kuzalisha waataam wengi
zaidi watakaolivusha taifa kuelekea kwenye mapinduzi ya sayansi na
teknolojia ya kisasa.
“Inatambulika
kuwa vijana ndio kundi kubwa katika jamii yoyote ile duniani na ndio
wenye nguvu zaidi za kufanya kazi kwa kuleta ubunifu kutoka na mawazo
mapya waliyonayo na ndio chachu ya mabadiliko ambayo huleta tija ya
kisayansi na kiteknolojia,” alisema Mavunde
“Dhana
ya ushirikishaji wa vijana katika masuala ya kidunia inatokana na
mchango mkubwa wa vijana walionyesha katika kuleta maendeleo ya mataifa
yao,”
Aliongeza
kuwa katika uongozi wa Awamu ya Tano, Serikali imeendelea kuweka
mikakati endelevu yenye malengo ya kuwawezesha vijana ikiwemo kuwapatia
mikopo yenye riba nafuu ambayo hutolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
unaosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, vilevile mikopo ambayo hutolewa na
halmashauri za wilaya zote nchini ambapo vijana hutumia fursa hiyo
kuanzisha au kuendeleza miradi mbalimbali inayowaingizia kipato.
Mheshimiwa
Mavunde alieleza kuwa Serikali pia ilianzisha Programu ya Kukuza Ujuzi
wa nguvukazi ya Taifa ambayo ni asilimia 56 ambapo kupitia programu hiyo
zaidi ya vijana 28,941 wamekwisha patiwa mafunzo ya Uanagenzi
“Apprentieship” katika fani za ufundi stadi, Vijana 20,432 wameweza
kurasimishiwa ujuzi wao uliopatikana nje ya mfumo rasmi “Recognition of
Prio Learning”, Vijana 5,975 wahitimu wa elimu ya juu wa fani mbalimbali
wamewezeshwa kupata mafunzo ya uzoefu kazi na pia kupitia programu hiyo
vijana 8,980 wamepatiwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kutumia teknolojia
ya Kitalu Nyumba “Greenhouse”.
Sambamba
na hayo, Naibu Waziri Mavunde alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana
kushiriki kwa wingi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Wawakilishi
na Madiwani ifikapo tarehe 28 Oktoba 2020 na watambue kuwa wao ni wadau
muhimu katika zoezi hilo n ani haki yao ya kikatiba.
“Vijana
ni wadau muhimu katika zoezi hili, hivyo kuwawezesha kwenda kupiga kura
ni haki yao waliyopewa na Katiba ya Nchi kushiriki katika shughuli za
uchaguzi kwa amani na utulivu na kamwe wasitumike vinginevyo,” alisema
Mavunde
Aidha
Mhe. Mavunde alisema kuwa Serikali pia imeendelea kuwawezesha vijana
kushiriki katika ngazi mbalimbali za maamuzi akitolea mfano mwaka huu
2020 zaidi ya asilimia 60 ya vijana wameweza kujitokeza kwa lengo la
kushiriki katika sehemu ya ustawi wa taifa.
“Ni
Dhahiri katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi
mahiri wa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ameonyesha Imani kubwa sana kwa vijana wenye sifa za uongozi
kuweza kushiriki kwenye uongozi kupitia teuzi mbalimbali na imeongeza
mihemuko kwa vijana kuweza kushiriki kwenye ngazi za maamuzi,” alisema
Mavunde
No comments :
Post a Comment