Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amekiri utekelezwaji wa miradi ya
kimkakati na maagizo mengine yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
Amesema
Rais Dkt. Magufuli alitoa maagizo mawili katika mradi wa nyumba za NSSF
uliopo Dungu; kwamba wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kigamboni waingie katika nyumba hizo agizo ambalo limeshatekelezwa na
nyumba 99 ambazo zimekamilika tayari zimepangishwa.
Jenista
alisema hayo baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua utekelezaji wa
maagizo ya Mhe. Rais Magufuli ambapo alianzia ujenzi wa barabara
inayounganisha Daraja la Nyerere, na kuongeza kuwa NSSF inafanya kazi
nzuri na ina uwezo mkubwa unaoweza kusaidia uwekezaji.
Naye,
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Salimu Matimbwa,
ambaye ni mmoja wa wapangaji wa nyumba za NSSF zilizopo Dungu, alisema
amepata nyumba ambayo hakuitegemea kama angeweza kupata kwa sababu ni
nzuri, imejengwa kisasa na inastahili kuishi binadamu yoyote.
Mkazi
wa Kigamboni, Felix John, aliishukuru Serikali kupitia NSSF kwa sababu
imewasaidia vijana kupata ajira katika mradi huo wa ujenzi barabara
inayounganisha Daraja la Nyerere.
Mjasiriamali Mwajuma Salumu Shukuru akiishukuru Serikali na NSSF, kwa kukamilisha ujenzi wa kipande cha barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni, na kuainisha kuwa kabla ya barabara hiyo ya lami walikuwa wanapata shida kubwa ya vumbi. Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki
Mkazi wa Kigamboni, Meja Mstaafu wa JWTZ, Adiel Raphael Kaay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ubora wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF Balozi Ali Iddi Siwa
No comments :
Post a Comment