Thursday, August 13, 2020

BAADA YA KUKOSA KURA ZA MAONI BALOZI KAMALA ATOA NENO


……………………………………………………………………..

Na Mwandishi Wetu.

Aliekuwa Mbunge Wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Kamala, ameahidi kuwa ataendelea

kutoa msaada wa kuwasomesha vijana elfu moja kupata mafunzo ya elimu ya ufundi stadi yatakayowawezesha  kujiajiri.

Akizungumza na waandishi wa habari  ,Balozi Kamala amesema kuwa atahakikisha anatimiza malengo hayo, kwa hali yoyote akiwa mbunge au akiwa mtu wa kawaida.

Balozi Kamala katika Uchaguzi wa kura za maoni alishindwa kutetea kiti  chake cha Ubunge katika jimbo la Nkenge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (Ccm).

Hatua  hiyo imewapa wasiwasi vijana ambao  wengi wao  wapo katika chuo cha ufundi stadi  cha Maendeleo ya wananchi Gera, kwa msaada wa Balozi Kamala.

Hata hivyo Katika kufanikisha adhma yake  ya kuwasaidia vijana wa jimbo hilo, Balozi Kamala, amefungua ofisi binafsi ambayo  itakayohusika na maswala ya kusimamia miradi aliyoianzisha kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi, ikiwemo huo wa kuwasomesha vijana elfu moja.

Kamala amesema mpaka sasa Mafunzo hayo ambayo yanatolewa kwa muda wa  miezi mitatu, mpaka sasa jumla ya vijana 140 wananufaika nayo ambapo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu vijana wengine 100 wataanza mafunzo hayo.

Mafunzo wanayopatiwa katika chuo hucho ni pamoja na   ufugaji nyuki, kilimo Cha mbogamboga, ushonaji, umeme wa  majumbani, computer na ujasiriamali.

 

No comments :

Post a Comment