……………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Halimashauri ya Kongwa Mkoani
Dodoma imeweka mikakati Madhubuti ya kuhamasisha wananchi wanahudumiwa
na kupata matibabu kwa gharama nafuu kwa kujiunga na mfuko wa
Bima ya
Afya ya Jamii ya CHF iliyoboreshwa ili kutimiza adhima ya serikali ya
Awamu ya Tano.
Kauli hiyo imebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Dkt. Omary Nkulo alipokuwa akizungumza na waandishi wa hapabri.
Aidha Dkt. Nkulo amesema kuwa
Halmashauri ya wilaya ya Kongwa ni moja ya Halmashauri iliyokuwa
ikifanya vizuri sana kwenye Bima ya CHF kutokana na mikakati ya
uhamasishaji waliojiwekea lakini pia ameahidi kama Halmashauri
kuendelea kufanya uhamasishaji ili watu wengi zaidi wajiunge na CHF
iliyoboreshwa.
“Kwa Kongwa tumejiwekea utaratibu
madhubuti wa Uhamasishaji na Timu yangu ya uhamasishaji chini ya Bwana
Amos,kwa kweli inafanya kazi nzuri sana,sasa hivi tunakwenda kuhamasisha
kwenye nyumba za Ibada,na muitikio ni mkubwa sana,watu wamekuwa
wakiuliza maswali na kujiunga na Bima hii,niwaambie tu wananchi wa
Kongwa, Serikali yao inawajali sana na ndio maana inataka kuwahudumia
kwa gharama nafuu hivyo wajitahidi kuwa na Bima ya CHF”ameeleza Dkt.
Omary.
Naye Mratibu wa CHF Wilaya ya
Kongwa Amos Erenest amesema kuwa wakina mama waliofika kwa ajili ya
kupatiwa huduma ya kliniki wamekuwa wakihamasishwa kujiunga na Bima
hiyo mwananchi akijiunga, kaya moja yenye watu sita kwa gharama ya
shilingi elfu 30.
Pia Erenest ameongezea kwa kusema
kuwakipindi mtu atakapo jiunga papo kwa papo anawezaa kuanza kupata
matibabu kwa gaharama hiyo nafu.
“Hivyo ndugu zangu wananchi kama
ilivyo kwa Sera ya Afya ya Serikali ya awamu ya Tano kwa kuwapenda
watanzania wake kuepukana na usumbufu wa matibabu ni vizuri tukawa na
Bima hii ya Afya yenye gharama nafuu, katika watu sita hao kila mmoja
anakuwa na kitambulisho chake”, ametoa wito Erenest.
Kwa Upande wake mnufaika wa CHF
iliyoboreshwa Neema Mazengo anasema kupitia Bima hiyo amekuwa akipata
matibabu mazuri na sambamba na kupata dawa kwa bei nafuu tofauti na
awali kabla ya kuwa na bima hiyo.
“Toka nijiunge na CHF mwezi wa
pili nimekua nikija hapa kituoni na Napata matibabu vizuri tu,vipimo na
dawa vyote Napata bure,kwa kweli imenisaidia sana yaani kuna utofauti
mkubwa sana kwa sasa na kabla sijawa na kadi hii,niwasihi tu wananchi
wengine ambao bado hawajakata Bima hii kwani ni gharama ndogo alafu
unatibiwa wewe na watu wengine sita kwa mwaka mzima”ameeleza Mazengo.
No comments :
Post a Comment