Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WATAALAMU
Wa masuala ya maendeleo wameendelea kuipongeza Tanzania na kutabiri
kuwa nchi hiyo itakuwa na uchumi mkubwa barani Afrika.
Hiyo
ni baada ya Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kuwa moja ya nchi
iliyofikia uchumi wa kati huku juhudi za Rais Dkt.John Magufuli
zikielezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia malengo hayo.
Profesa
David Himbara kutoka Chuo cha Centennial , Toronto nchini Canada ambaye
pia ni mchambuzi wa masuala ya kimataifa yahusuyo maendeleo kupitia
makala yake ya "The African Report" ameipongeza Tanzania kwa kufikia
uchumi wa kati na hiyo imechagizwa na uimara wa hali ya kisiasa pamoja
na mabadiliko yaliyofanywa ndani ya miaka mitano ya Rais Dkt. Magufuli.
Ni
Julai Mosi mwaka huu, licha ya ulimwengu kukumbwa na janga la Corona
Tanzania ilipokea taarifa nzuri ya kuwa moja ya nchi iliyofanikiwa
kuingia katika uchumi wa kati ikiwa ni miaka mitano kabla ya malengo
hayo yaliyopangwa kufikiwa mwaka 2025.
Katika
makala hiyo imeelezwa kuwa Tanzania imekua moja kati ya nchi 5
zinazozalisha dhahabu barani Afrika na hata baada ya anguko la miaka
mitano nchi hiyo sasa inazalisha saruji, vifaa mbalimbali vya ujenzi,
na mashine rahisi na hiyo ni pamoja na uwepo wa viwanda mbalimbali
ikiwemo nguo ambavyo pia vimetoa ajira kwa mamia ya vijana.
Aidha
imeelezwa kuwa Tanzania imepiga hatua katika uzalishaji na usafirishaji
wa bidhaa kwa nchi za Burundi, Rwanda, Congo DRC, Uganda na Zambia.
Pia
imeelezwa kuwa huduma za simu, mabenki na miradi ya ujenzi imeshuhudia
ukuaji mkubwa zaidi huku mji wa kibiashara Dar es Salaam ukitajwa kuwa
mji mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Uchambuzi
huo umeeleza matumizi sahihi ya rasilimali pamoja na ushirikishwaji wa
vyombo vya habari imechangia kwa kiasi kikubwa kuyafikia maendeleo hayo
huku ikielezwa kuwa shughuli za kilimo na shughuli za viwanda
utanipeleka nchi hiyo katika hatua nyingine kwa siku zijazo.
No comments :
Post a Comment