WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii na Wazee Ummy Mwalimu wa kati kati akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Pwani kushoto
kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kabla ya kwenda
kufunga kambi wa wagonjwa wa Corona katika eneo la Lulanzi Wilayani
Kibaha,(Picha na Victor Masangu).
**************************
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAZIRI wa Afya
Maendeleo ya Jamii na Wazee Ummy Mwalimu amefunga kambi ya
wagonjwa wa
Corona iliyokuwa Lulanzi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Akifunga
kambi hiyo jana ambapo alisema, kati ya kambi 85 zilizokuwa zinahudumia
wagonjwa wa Corona zimebaki 11 ambazo nazo zinaendelea kufungwa siku
zijazo kutokana na ugonjwa huo kuendelea kutokomea hapa nchini.
Aliwasihi
wananchi kuacha kujibweteka na kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa
huo katika maeneo mbalimbali ili kuepuka kupata maambukizi mapya.
“Tumefunga
kambi 74 hadi sasa na hii hapa Lulanzi ilikuwa ni Kati ya kambi kubwa
ambayo ilikuwa inapokea wagonjwa wengi na leo naifunga rasmi kwani
mgonjwa wa mwisho hapa aliruhusiwa Mei 26 hakuna mwingine aliyepokelewa
hadi leo” alisema
Aidha Waziri
Ummy aliwataka wakazi wa Kibaha kufika katika Hospitali ya Wilaya kupata
huduma na kuondoa hofu ya kuwa kituoni hapo bado kuna wagonjwa wa
Corona.
Alisema, wananchi wanatakiwa kuondoa hofu kwani majengo yote yamefanyiwa usafi baada ya wagonjwa kuondoka katika Hospitali.
” Lulanzi sio
tena kambi ya wagonjwa wa Corona , wananchi ondoeni wasiwasi na mfike
kupata huduma za afya, tusikimbilie Tumbi ile ni Hospitali ya Rufaa
tungependa ibaki kutoa huduma za hadhi ya Rufaa” alisema Ummy.
Alitumia
nafasi hiyo pia kutoa wito kwa Halmashauri ya mji wa Kibaha kusimamia
utoaji wa huduma za viwango vinavyostahili kwa wagonjwa.
Akiongea
katika Hospitali hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka
alimshukuru Rais Pombe Magufuli kwa Hospitali hiyo ambayo imemaliza
uhitaji wa Hospitali ya Wilaya aliyokuwa akiiomba kwa zaidi ya miaka
saba iliyopita.
Koka aliwataka wananchi kufika kutibiwa katika Hospitali hiyo ambayo imeondoa kilio cha uwepo wa Hospitali ya Wilaya .
Alisema
changamoto iliyopo katika Hospitali hiyo kwasasa ni pamoja na ubovu wa
barabara na gari la wagonjwa ambalo Waziri Ummy aliahidi litapatikana
hivi karibuni.
Mganga mkuu
wa Halmashauri ya mji wa Kibaha Tulitweni Mwinuka alisema, Hospitali
hiyo imeanza kutoa huduma za kawaida kwa wagonjwa Juni 6 na kwamba jamii
bado ina Mashaka kufika katika Hospitali hiyo.
No comments :
Post a Comment