Mkurugenzi wa uendeshaji
UTT-AMIS Issa Wahichindena akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa
kituo cha kuhudumia wawekezaji cha UTT-AMIS katika jengo la Ngorongoro,
jijini Arusha, anayeangalia (Katikati) ni meneja wa uhusiano katika
kitengo cha uangalizi wa amana katika benki ya CRDB, Mary Mponda (Picha
na Pamella Mollel)
Meneja wa Uhusiano, kitengo cha
uangalizi wa amana, katika Benki ya CRDB Mary Mponda (Kulia),
akizungumza katika uzinduzi wa UTT Arusha, huku Meneja wa Tawi la TFA la
benki ya CRDB Arusha Ronald Paul (Kushoto) akifuatilia kwa makini
(Picha na Pamella Mollel)
Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa
UTT-AMIS, Daudi Mbaga akizungumza na waandishi wa habari wa kati wa
hafla hiyo (Picha na Pamela Mollel)
Picha ya Pamoja ya baadhi ya
wafanyakazi wa UTT-AMIS na wafanyakazi wa benki ya CRDB mara baada ya
uzinduzi wa kituo cha kuhudumiawawekezaji Arusha (Picha na Pamella
Mollel).
**********************************
Na Pamela Mollel, Arusha
Kampuni ya Serikali inayohusika na
Uanzishaji na Uendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini,
UTT-AMIS imezindua tawi lake la tatu jijini Arusha baada ya lile la
Dodoma katika mkakati wake wa kusogeza huduma karibu zaidi na
wananchi.
“Tunafungua rasmi kituo cha
kuhudumia wawekezaji wetu katika jiji la Arusha, hii ni ikiwa ni
ushahidi wa maendeleo mazuri katika sekta ya uwekezaji kwa wananchi wa
kawaida, Tanzania zikiwa ni juhudi kubwa za serikali ya awamu ya tano
chini ya uongozi wa Rais John Maguifuli,” alisema Mkurugenzi wa
Uendeshaji wa UTT-AMIS, Issa Wahichindena.
Akizungumza katika ufunguzi wa
kituo hicho katika jengo la Ngorongoro Conservation Center, lililopo
katikati ya jiji, Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kwa kuwekeza katika
mifuko hiyo wawekezaji wananufaika na unafuu wa gharama za uwekezaji.
Naye mkuu wa Masoko na Uhusiano
wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga amesema kuwa kuna umuhimu wa wananchi kuongeza
thamani ya akiba zao kwa kuwek
eza fedha katika mifuko ili kupata faida kubwa badala ya kuziacha benki ambako riba zake huwa ndogo.
Katika uzinduzi huo pia
walikuwepo maafisa watendaji wa benki ya CRDB, akiwemo Meneja wa
Uhusiano, kitengo cha uangalizi wa amana, Mary Mponda ambaye alisema
kuwa taasisi yao kwa sasa ina matawi zaidi ya 280 nchini kote na kuwa
katika nafasi nzuri ya kusimamia mifuko ya uwekezaji nchini.
No comments :
Post a Comment