Friday, July 3, 2020

WAZIRI KAIRUKI AWATAKA TPC KUZALISHA SUKARI YA VIWANDANI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angellah Kairuki akizungumza na Menenjimenti ya Kiwanda cha Sukari -TPC kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro (Hawapo pichani)  alipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake .
Afisa Mtendaji -Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC-Jafary Ally akielezea jambo mbele ya Waziri Kairuki alipotembelea kiwandani hapo .
Afisa Mtendaji -Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC-Jafary Ally  (Wa pili kutoka kulia) akimuongoza Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angella Kairuki kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho.
Sehemu ya Kiwanda cha Sukari cha TPC 
Waziri Kairuki akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi a kiwanda cha Sukari cha TPC namna ambavyo machine ya kuzalisha umeme kiwandani hapo inafanya kazi .
Waziri Kairuki na Viongozi wengine alioambatana nao wakishuka katika moja ya ngazi zilizopo kiwandani hapo .
Sehemu ya Mabehewa yanayotumika kusafirisha Miwa kutoka mashambani na kuifikisha katika eneo la kiwanda .
Waziri Kairuki akitizama namna ambavyo sukari inawekwa kwenye mifuko kabla ya kwenda kwa mtumiaji wa mwisho .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angela Kairuki akitoka katika eneo la kiwanda hicho mara baada ya kujionea uzalishaji unavyofanyika katika kiwanda hicho .
Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro .
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia uwekezaji, Angela Kairuki,ameutaka uongozi wa
Kiwanda cha Sukari cha TPC, kilichopo Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro,
kuangalia uwezekano wa kuanza uzalishaji wa Sukari ya viwandani, ili kuondoa
adha ya kuagiza sukari hiyo nje ya nchini.
Kairuki alisema mpaka
sasa hakuna mzalishaji wa sukari za viwandani nchini na kwamba serikali huagiza
zaidi ya Tani 155,000,na kwamba endapo TPC wataanza uzalishaki huo, watasaidia
upatikanaji wa sukari hiyo kwa urahisi.
“Niwashauri TPC,
kuangalia ni namna gani,mnaweza kuzalisha sukari za viwandani, tukitambua bado
hatuna mzalishaji hata mmoja hapa nchini, ambaye anazalisha sukari za
viwandani,tunaagiza zaidi ya tani 155,000 za sukari hii, tunamini mkileta
mitambo, mnaweza kuzalisha na kuweza kupata sukari hiyo hapa
nchini”alisema Kairuki
Mbali na hilo Kairuki
amewataka wawekezaji, kuendelea kutazama fursa za uwekezaji zilizopo nchini na
kuwekeza katika nyanja mbalimbali, ili kufanikisha malengo ya kuifanya Tanzania
kuwa nchi ya Viwanda.
Alisema bado kuna
mahitaji makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini, na bidhaa nyingine zinaagizwa nje
ya nchi, hivyo ipo haja kwa wawekezaji kujitokeza na kuwekeza katika nyanja
mbalimbali, hatua ambayo itapanua wigo wa ajira kwa watanzania na hata kuinua
pato la taifa.
“Mahitaji bado ni
makubwa nchini, kuna changamoto ya chupa za kioo,Chupa za Plastiki na bidhaa
nyingi tunaagiza nje, sasa angalieni, mkiona kuna fursa, serikali tupo tayari
kutoa ushirikiano, ili muweze kupanua wigo wa uwekezaji”alisema Kairuki.
Akizungumza Ofisa
mtendaji utawala katika kiwanda cha TPC, Jaffari Ally,alisema mpaka sasa
kiwanda hicho kina sukari zaidi ya tani 3,300 ambazo zipo kwenye Ghala, na
kuwatoa hofu watanzania, kuwa hakuna tena upungufu wa sukari nchini.
“Tuwatake
wasambazaji wakubwa na wauzaji wa rejareja wa sukari nchini, kuacha kuwalangua
wananchi na kuhakikisha wanauza sukari kwa bei ya awali ya kabla ya kufungwa
kwa msimu, maana kwa sasa sukari inayouzwa inazalishwa hapa nchini na hakuna
inayoagizwa nje ya nchi”alisema.

No comments :

Post a Comment