WATANZANIA
100 walilondoka nchini kinyume cha sheria na kutokomea Afrika Kusini,
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na
shtaka la kuondoka nchini bila kufuata taratibu za uhamiaji.
Watuhumiwa
hao, ambao wengi wao wameonekana kuwa ni Vijana wamesomewa mashtaka yao
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ambapo wote wamekiri kutenda
kosa hilo na wameiomba mahakama iwasamehe.
Hata
hivyo, Hakimu Simba amesema kuwa haoni faida yoyote ya kuwapeleka
watuhumiwa hao gerezani haswa katika kipindi hiki ambacho kuna gonjwa
hatari la Corona....
"Sioni
faida yoyote ya kuwapeleka gerezani lakini mahakama inawapa onyo kali
na inawaachia kwa masharti msirudie kutenda kosa hili kwa miezi sita,
amesema Hakimu Simba.
Mapema wakisomewa shtaka lao na wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji GodfreyNgwijo.
Inadaiwa,
Julai 3, 2020 huko katika uwanja wa Ndege wa Juliys Nyerere uliopo
Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote 100 walikutwa wakiwa
wameondoka nchini kinyume cha sheria bila kufuata utaratibu wa kutoka
na kuelekea Afrika Kusini.
Wakisomewa
Maelezo ya awali imedaiwa katika tarehe zisizojulikana washtakiwa hao
waliondoka nchini bila kufuata utaratibu na kwamba Julai 3 mwaka huu
watuhumiwa walirudishwa nchini Tanzania baada ya uchunguzi na
kugundulika kuwa ni wahamiaji haramu.
No comments :
Post a Comment