Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe (kulia), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko aliyefika kwenye banda la PSSSF viwanja vya Julius Nyerere
Meneja
wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe, akibadilishana mawazo na Afisa
Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kulia) na Afisa Uhusiano wa
Mfuko huo, Bw. Meseka Kadala
Afisa
Matakelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald Meeda (kushoto),
akimfafanulia masuala mbalimbali ya huduma za Mfuko, mwanachama huyo
aliyepata fursa ya kutembelea banda la PSSSF.
Afisa
wa huduma kwa wateja mwandamizi wa PSSSF, Bi. Nelusigwa Mwalugaja
(kushoto), akimfafanulia mwanachama huyu kuhusu michango yake.
Afisa
Mafao PSSSF, Bw.Abddallah Juma Adam (kulia), akitoa huduma kwa
mwanachama aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya
Julias Nyerere maarufu Sabasaba.
Afisa Matekelezo PSSSF, Bi. Zainab Ndullah (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo.
|
Mwanasheria
wa PSSSF, Bw. David Mnkande (kulia), akifafanua kuhusu huduma za
kisheria za Mfuko huo kwa wanachama hawa waliotembelea banda la PSSSF.Na mwandishi wetu, Sabasaba.
WANACHAMA
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa
kufika kwenye ofisi za Mfuko huo zilizoenea katika mikoa yote nchini ili
kuhakiki taarifa zao.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 3, 2020, Meneja wa PSSSF mkoa
wa Temeke, James Mlowe alisema mwanachama akifika kwenye ofisi yoyote ya
PSSSF utaratibu na mahitaji yako vile vile hivyo amewahimiza kufanya
hivyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kutohakiki
taarifa.
Lakini
pia amewaalika wanachama watakaotembelea kwenye viwanja vya Julius
Nyerere kwenye maonesho hayo ya biashara maarufu kama sabasaba, wataweza
kujipatia huduma zote kama zinavyotolewa kwenye ofisi za Mfuko kwenye
mikoa yote nchini.
“Tulichofanya
mwaka huu tumehamisha miundombinu na vifaa vyote vya kutoa huduma
vinavyopatikana kwenye ofisi zetu ikiwemo makao makuu, hivyo mwanachama
anapofika kwenye banda letu anapata huduma zote ikiwemo, taarifa za
michango, mafao, pensheni na mafao yanayotolewa na Mfuko” alifafanua Bw.
Mlowe.
Maonesho
hayo yaliyoanza Julai 1, 2020 yamefunguliwa rasmi Ijumaa Julai 3, 2020
na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Uchumi wa viwanda, ajira na biashara endelevu”. |
No comments :
Post a Comment