Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya
Uondoshaji wa Mashauri ya Jinai ambaye pia ni Msajili wa Mahakama Kuu
ya Tanzania, Sharmillah Sarwatt (kushoto) na Katibu wa kikao hicho Naibu
Msajili Mkuu Mwandamizi wa Mahakama kuu ya Tanzania Masijala Kuu Mhe
Messe Chaba (kulia).
Mkurugenzi wa Menejimenti ya
Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith Kamugisha
akitoa taarifa leo ya uendeshaji wa mashauri ya jinai katika kipindi
cha Januari, mwaka huu hadi Julai Moi, mwaka huu kwenye kikao kazi cha
robo mwaka ya pili ya mwaka wa kimahakama cha mwaka huu kilichohusisha
wadau wa Haki Jinai.
Mwakilishi kutoka katika ofisi ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), ambayo
imewakilishwa na Naibu Kamishna wa Polisi. Bw.Saleh Ambika akifafanua
jambo.
Kamishna Msaidizi
wa Magereza, Bw,Willington Kamuhuza,(kushoto) akizungumza jambo kwenye
kikao hicho. (Kulia ) ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa
Mashauri Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith Kamugisha.
( PICHA NA MAGRETH KINABO – MAHAKAMA)
…………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo na Innocent Kansha – Mahakama
Jumla ya mashauri ya jinai 24,698
yalifunguliwa katika ngazi zote za Mahakama nchini nzima isipokuwa
Mahakama za Mwanzo kati ya hayo 25,950 yalisikilizwa sawa na asilimia
105.06 ya
mashauri yote yaliyofunguliwa katika kipindi cha Januari hadi
Julai Mosi, mwaka huu.
Akizungumza wakati akitoa
taarifa hiyo leo ya uendeshaji wa mashauri hayo katika kipindi hicho,
kwenye kikao kazi cha robo mwaka ya pili ya mwaka wa kimahakama cha
mwaka huu kilichohusisha wadau wa Kamati ya Kitaifa ya Haki Jinai.
Mkurugenzi wa Menejimenti ya
Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Deusdedith Kamugisha
Mahakama hivi sasa ina uwezo wa kusikiliza mashauri yote yanayoingia
mahakamani ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati.
‘‘Taarifa hii inaelezea hali
ya ufunguaji na usikilizaji wa mashauri ya jinai kwa kipindi cha Januari
hadi Julai Mosi, 2020 kwa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Mahakama za
Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya nchi nzima.“Kwa upande wa Mahakama
ya Rufani Tanzania, jumla ya mashauri ya jinai 297 yalifunguliwa na
mashauri 210 yalisikilizwa sawa na asilimia 70.7 ya mashauri yote
yaliyofunguliwa katika kipindi hicho,’’ alisema Kamugisha huku akisema
wastani wa mzigo wa mashauri ni 737 kwa jopo la majaji wa tatu.
Alisema Mahakama Kuu ya
Tanzania, mashauri ya jinai 2,561 yalifunguliwa na 2,618 yalisikilizwa
sawa na asilimia 102.2. Wastani wa mzigo wa mashauri ni 345 kwa kila
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kamugisha alisema katika
Mahakama za Hakimu Mkazi jumla ya mashauri 5,338 yalifunguliwa, 5,566
yalisikilizwa sawa na asilimia 104.3 ya mashauri ya jinai
yaliyofunguliwa. Hivyo wastani wa mzigo wa mashauri ni 198 kwa kila
Hakimu.
“Mahakama za Wilaya mashauri
16,169 yalifunguliwa, mashauri 17,254 yalisikilizwa sawa na asilimia
97.5.Hadi kufikia Julai Mosi, 2020 wastani wa mzigo wa mashauri kwa
Mahakama za Wilaya ni 96 kwa kila Hakimu,”alisisitiza
.
Aliongeza kwamba mashauri 333 yalifungiliwa katika Mahakama za Watoto, 302 yalisikilizwa sawa na asilimia 90.6.
Kwa upande wa ofisi ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, ambayo
imewakilishwa na Naibu Kamishna wa Polisi Bw.Saleh Ambika alieleza kuwa
lengo kuu la ofisi yake ni kuhakikisha upelelezi wa makosa ya jinai
unafanyika na unakamilika kwa haraka zaidi kadri iwezekanavyo.
“Upelelezi wa makosa ya jinai
una hatua mbalimbali na unahusisha taasisi mbalimbali za mfumo wa haki
jinai kuna wakati mwingine Polisi wanahitaji kupata ripoti zinazotoka
mamlaka nyingine kukamilisha upelelezi ili kumfikisha mtuhumiwa
mahakamani kwa wakati,” alisema Ambika.
Alifafanua kuwa upelelezi
unaohusisha sampuli za kitu fulani, Kitengo cha Upelelezi lazima
kishirikiane na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakatiKmwingine sio
rahisi kupata ripoti kwa kadri ya matarajio ya upelelezi wako, pia
taasisi hiyo inataratibu zake za kiuchunguzi ili kukamilisha hilo,
Ambike alisema ushirikiano
wadau hao upo kwa kiwango cha kutosha, hivyo hilo ndio lengo la kamati
hiyo ni kuisaidia Mahakama ya Tanzania kufikia ajenda ya kupunguza
mlundikano wa mashauri mahakamani.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka
Idara ya Huduma za Uangalizi kwa wafungwa wanaotumikia vifungo vya nje
ya Magereza, Bw. Charles Nganze alisema wafungwa 706 walitumikia adhabu
mbadala ya kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo ya Makaburi ya
Kinondoni, mabwawa ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam
(DAWASA) , wizara na zahanati mbalimbali.
Naye Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Bw,Willington Kamuhuza, alishukuru jitihada zilizofanywa na
wadau hao zimesaidia kupunguza msongamano wafungwa kwa asilimia
0.73.Pia aliongeza kwamba kwa kutumia Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) jumla ya mikoa 16 iliyo na magereza mashauri hayo
yamesikilizwa kwa njia ya Mahakama Mtandao baada ya kuwezeshwa kuwa na
vifaa vya TEHAMA kutoka Mahakama ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Uondoshaji wa Mashauri ya Jinai, ambaye pia ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt alisema lengo kikao hicho ni kutathmini utendaji kazi na kupanga mikakati ya kupunguza mlundikano wa mashauri ya aina hiyo.
No comments :
Post a Comment