Mhandisi mkazi wa mradi wa JNHPP Eng. Mushubila Kamuhabwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi
Muonekano wa njia nyingine ya
kuchepusha maji (diversion tunnel eneo la mradi wa ujenzi wa bwawa la
umeme la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) katika hatua mbalimbali
Vijana wakiwa wamebeba nondo
wakati kazi ya ujenzi wa njia ya ardhini ya kuchepucha maji (diversion
tunnel) eneo la mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere
(JNHPP-MW2115) ikiendelea
Mashine zikichoronga mlima na
malori yakibeba kifusi kwenye bonde la mto Rufiji eneo la mradi wa
ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115)
…………………………………………………………………………
Na mwandishi wetu, JNHPP
HATUA zote nane
(8) za utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji la
Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) kwenye bonde la mto Rufiji unaendelea kwa
kasi inayohitajika, Mhandisi mkazi wa mradi huo Eng. Mushubila
Kamuhabwa amewaambia waandishi wa habari kwenye eneo la mradi Julai 17,
2020.
Eng. Kamuhabwa ametaja hatua hizo kuwa ni ujenzi wa njia kubwa ya ardhini ya mchepuko wa maji (diversion tunnel), sehemu ya kufua umeme (power house), ukuta utakaotengeneza bwawa, eneo la kupokelea umeme unapozalishwa (Switch yard), power intake, barabara na madaraja, saddle dams nne na kuchakata mawe yanayotumika kutengeneza zege na mahitaji mengine.
“Mradi huu wa
JNHPP una miradi mingi ndani yake na yote iko katika hatua mbalimbali
na hatua hizo kama nilivyozitaja kwa pamoja ndiyo zinajenga mradi mmoja
wa Julius Nyerere Hydro Power Project Megawati 2115 katika hilo ujenzi
unaendelea katika maeneo yote hayo, mafundi wako kazini na wanaendelea
na ujenzi kwa kasi kubwa kama inavyohitajika.” Alisema Eng. Kamuhabwa.
Alisema jambo la
kufurahisha tayari mradi umeanza kuchangamsha uchumi wa nchi na kutolea
mfano wakati wakiweka zege kwenye njia ya kuchepusha maji (diversion
tunnel, zaidi ya tani 200 za nondo zimetumika hii inafaidisha viwanda
vyetu hapa nchini lakini pia wananchi wanaokaa vijiji vinavyozunguka
eneo la mradi wanafaidika kwa namna mbalimbali ikiwwemo miundombinu
wezeshi kama vile umeme unaotoka Morogoro kuja hapa umepitia kwenye
vijiji kadhaa natayari baadhi yao wameanza kufaidika na umeme huo.”
Alisema na kuongeza…Lingine zaidi ya vijana wa Kitanzania wapatao 4,000
kutoka maeneo mbalimbali nchini hususan yale yanayozunguka eneo la mradi
wameajiriwa na wanashiriki katika mradi kwa ari kubwa.
“Tunatarajia idadi hiyo ya ajira ikaongezeka hadi kufikia watu 6,000 mradi utakapofikia hatua ya juu peak.” Alisema Eng. Kamuhabwa.
Kwa upande wao
baadhi ya wanakijiji wa Kisaki kilomita 60 kutoka eneo la mradi
wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Magufuli kwa kuwaletea mradi huo kwani tayari manufaa yake wameanza
kuyaona.
“Kisaki
inakuja juu, tuna uhakika mradi ukimalizika Kisaki itakuwa kama
Morogoro, kwa sasa biashara inakuwa kwa kasi sana tofauti na hapo awali,
mfano mchele tunauza kwa kilo shilingi 1,600/= tofauti na hapo awali
tulikuwa tunauza shilingi 500/= bei ya juu kabisa shilingi 1,000/=, watu
wameongezeka sana.” Alisema mwanakijiji wa Kisaki Ali Matumbo na
kuongeza…umeme nao tayari umefika kijijini kwetu, shule imepata umeme
kwa hivyo tunafuraha sana kwa ujio wa mradi huu na tunampongeza sana
Rais wetu Magufuli.
Naye mwanakijiji
mwingine Bi. Asha Said alisema, anauhakika hata barabara nzuri itajengwa
kutokana na mradi huo na anafurahi kuona wageni wengi wanafika Kisaki
na hivyo biashara zao zimechangamka.
Naye mwanakijiji
mwingine Hassan Mohammed Ngozi alisema, anayo matumaini makubwa kwa hali
anavyoiona hivi sasa hapo Kisaki, mradi utakapokamilika watakuwa na
Kisaki mpya.
“Kwetu sisi
ongezeko la watu hapa Kisaki limekuwa na faida kubwa………..watu wakienda
kufanya kazi huko kwenye mradi wanakuja hapa kijijini wananunua bidhaa
zetu na sisi tunapata pesa haya ni manufaa makubwa kwetu.” Alisema Bw.
Ngozi.
No comments :
Post a Comment