………………………………………………………………………..
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia SUZY KENNETH KASITEJETA [19] Mkazi wa
Dar es Salaam kwa
tuhuma za mauaji ya LINUS JAMES MAGESA [21] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Kitengo cha Biomedical mwaka wa
kwanza na Mkazi wa Ikuti kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kifuani.
Ni kwamba mnamo tarehe 17.07.2020
majira ya saa 22:00 Usiku huko eneo la Ikuti lililopo Kata na Tarafa ya
Iyunga, Jijini Mbeya SUZY KENNETH KASITEJETA [19] na LINUS JAMES MAGESA
[21] ambao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi waligombana na kupelekea
LINUS JAMES MAGESA kujeruhiwa sehemu za kifuani kwa kuchomwa kitu chenye
ncha kali na SUZY KENNETH KASITEJETA hali iliyopelekea kukimbizwa
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.
Leo tarehe 18.07.2020 majira ya
saa 00:05 Usiku LINUS JAMES MAGESA [21] alifariki dunia akiwa anapatiwa
matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni
wivu wa kimapenzi. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa wapenzi hao walikuwa
wakigombana mara kwa mara. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara
baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
WITO:
Ninatoa wito kwa jamii kutofumbia
macho ugomvi unatokea mbele yao kwa kudhani ni kitu cha kawaida na kukaa
kimya, ni wito wa Jeshi la Polisi kwa jamii kutoa taarifa mapema kwa
Watendaji wa Kata au Wenyeviti wa Mitaa ambao ni walinzi wa amani katika
maeneo yao ili waweze kuchukua hatua za awali kupitia baraza la
usuluhishi la Kata au Mtaa.
KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia DICKSON KABUJE [32] Mkazi wa Ikumbi akiwa na mali mbalimbali za wizi.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe
17.07.2020 majira ya saa 14:00 Mchana huko Kijiji cha Ikumbi, Kata ya
Utengule – Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa
Mbeya na katika upekuzi alikutwa akiwa na mali za wizi ambazo:-
- Spika kubwa 02,
- Redio Sub-Woofer 01 na Spika zake,
- Stablizer 01, m
- Mtungi mkubwa wa gesi Mihani 01,
- Deki 02 za Singsung,
- Godoro 01 Super Banco.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
No comments :
Post a Comment