******************************
Grace Semfuko, Dar es Salaam
Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC
katika kipindi cha January 2016 hadi Juni 2020 kimefanikiwa kusajili
miradi 1,312 ya Uwekezaji yenye mtaji wa thamani ya Dola za Marekani
Bilioni 20 ikiwa ni takribani Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania, miradi
hiyo inatoa ajira kwa
watanzania 178,101.
Katika usajili huo Sekta ya
usindikaji na uzalishaji wa Viwanda iliongoza kwa asilimia 54 ya miradi
yote na kutoa ajira ya watanzania 67,992.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya Kituo cha Uwekezaji
Tanzania katika kipindi cha miaka mitano madarakani ya Rais Dkt John
Pombe Magufuli, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Bw.
Geoffrey Mwambe amesema mafanikio hayo yanatokana na uongozi thabiti wa
Serikali ya sasa.
“Katika awamu hii ya Magufuli,
TIC imeendelea kutekeleza mpango mkakati wa miaka mitano, tulikuwa na
Dira ya kufikia Kituo Bora kabisa Duniani kwa kuvutia Uwekezaji
endelevu” alisema
Aliongeza kuwa Serikali ya
Tanzania inao uwezo mkubwa sana wa kufanya maendeleo ya kasi na kwamba
ndani ya miaka mitano tu hali ya uchumi na maendeleo ya Taifa
yamebadilika kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyotarajiwa.
*”Watanzania tunapaswa
kujivunia, ndani ya miaka mitano tumebadili kabisa hali yetu ya uchumi
na maendeleo ya Taifa yamekuwa kwa kasi sana, watu wengi wanaokuja
hawaamini kuwa hii ni Tanzania, wanadhani ni ile Tanzania ya awali
ambayo hatukuwa na uwezo wa kujenga miundombinu yetu wenyewe kama Reli
ya kisasa ya Standard Gauge na mengineyo, wanabaki tu kuhoji Tanzania
mnaweza? Na sisi tunasema ndio! Tunaweza” alisema Mwambe.
Alizungumzia pia uboreshwaji
wa TIC kwenye eneo la huduma za mahala pamoja (One Stop Facilitation
Centre) akisema zimeboreshwa na kuongezwa idadi ya Taasisi
zinazohudumia Wawekezaji kutoka Taasisi saba Mwaka 2015 na kufikia
Taasisi kumi Mwaka 2020 huku idadi ya watumishi kwenye eneo hilo
wakiongezeka kutoka 14 hadi 25.
Kuhusu kuongeza huduma za
Uwekezaji kwenye maeneo yote nchini, Mwambe alisema Ofisi za Kanda za
TIC zimeongezeka kutoka Kanda tatu Mwaka 2015 hadi kufikia Saba Mwaka
2020 na kuzitaja Kanda hizo kuwa ni pamoja na Kanda ya Ziwa, Kanda ya
Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya
Kaskazini, Kanda ya Mashariki na Kanda ya Magharibi.
Aidha alizungumzia pia hatua
ya TIC ya kuimarisha kamati ya Taifa ya uwezeshaji Uwekezaji (NIFC)
ambayo inahusisha Wakuu wa Taasisi za Serikali zinazotoa vibali na
leseni mbalimbali za Uwekezaji yenye jukumu la kusaidia kuondokana na
changamoto za Sekta hiyo kwenye maeneo yanayosimamiwa na Taasisi hizo.
Katika hatua nyingine Mwambe
amesema TIC imeboresha mifumo ya kuchakata na kutoa vibali kwa njia ya
mtandao ikiwepo utoaji wa cheti cha vivutio, usajili wa kampuni pamoja
na vibali vya kazi na ukaazi pamoja na kuwa na mkakati wa pamoja wa
kushirikiana kwenye shughuli zote za uhamasishaji Uwekezaji na Biashara.
Mwambe hakuacha kuzungumzia
tafiti zinazofanywa na Kituo hicho ambapo amesema ulifanyika Utafiti
kuhusu mienendo ya mitaji ya Uwekezaji toka nje ili kubaini hali halisi
ya ukuaji, fursa na changamoto za kisekta ili kuziboresha huku akizitaja
tafiti hizo kuhusika kwenye maeneo ya Kilimo, Mifugo, Viwanda nq
Mazingira ya Biashara kwa ujumla.
Katika mkutano huo na
Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwambe pia alitoa matokeo ya
tafiti za athari za Uwekezaji zilizofanywa kufuatia kuibuka kwa ugonjwa
wa Homa kali ya Mapafu- COVID-19 kwa Uwekezaji wa miradi iliyosajiliwa
na TIC huku alitaja sekta ya Utalii na Viwanda vya uchakataji
vinavyotegemea malighafi toka nje ya Nchi.
Alisema katika kipindi cha
COVID-19 TIC iliendelea kufanya kazi kwa ustadi mkubwa na kuboresha
mifumo ya utendaji kazi kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa Sekta ya
afya.
Mwisho.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC
katika kipindi cha January 2016 hadi Juni 2020 kimefanikiwa kusajili
miradi 1,312 ya Uwekezaji yenye mtaji wa thamani ya Dola za Marekani
Bilioni 20 ikiwa ni takribani Shilingi Trilioni 46 za Kitanzania, miradi
hiyo inatoa ajira kwa watanzania 178,101.

No comments :
Post a Comment