Sunday, July 12, 2020

TIBIA MAJI YENYE MADINI YANAYOATHIRI MENO NA MIFUPA, TEMBELEA MAONESHO YA SABASABA


 Meneja mradi kutoka kitengo cha uhandisi rasilimali maji, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Fanuel Ligate akielezea aina mbalimali za udongo na miamba inayoweza kutoa madini ya Fluoride pamoja na Arsenic kwenye maji ambayo yana madini hayo.
 Baadhi ya udongo na miamba inayoweza kutoa madini yanayoharibu meno na mifupa.
Meneja mradi kutoka kitengo cha uhandisi rasilimali maji, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Fanuel Ligate akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya sabasaba.

Na mwandishi wetu, Globu ya Jamii
TABASAMU lenye mwonekano wa meno meupe yasiyo na rangi rangi (kutu) inaletwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamekuja na teknolojia mbadala la kuchuja maji kuondoa madini ya Arsenic na Fluoride yanayoathiri meno na mifupa.

Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kipitia kitengo cha Uhandisi Rasilimali maji katika msimu wa Sabasaba amekuja na teknolojia inayo saidia kuimarisha mifupa na meno yaliyoathiriwa na unywaji na matumizi ya maji yenye kimikali.

 Akizungumza na waandishi wa Michuzi blog na Michuzi TV katika maonesho ya 44 ya biashara katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, Meneja mradi kutoka kitengo cha uhandisi rasilimali maji, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Fanuel Ligate  amesema kuwa amesema kuwa ili kugundua kama meno yameathirika dalili za awali ni kuona meno yamepata kutu.

"Mtu anavyoendelea kunywa maji yenye madini haya mifupa inaweza kuwa laini zaidi na inapinda na kuvunjika."

Amesema madhara hayo ya mifupa na meno hayatibiki kwahiyo njia pekee ya kuondoa maradhi hayo ni kujikinga na madini hayo ni kutumia teknolojia ya kuyaondoa madini hayo kwenye maji kabla maji  hajanywewa.

"Mfumo wetu wa chujio ambao tumeuleta hapa unatumika kuchuja maji kwa njia lahisi ambapo kama mtu anakisima chake cha maji au tenki la maji anapampu maji yapite katika chujio hili na yakifika kwenye hatua za mwisho maji yanakuwa kwenye kiwango ambacho kinakubalika na shirika la Afya Duniani pamoja na TBS."Amesema Ligati

Hata hivyo amesema kuwa teknolojia inayotumika kuondoa madini ya Fluoride na Arsenic katika maji ni ya hapa hapa nchini

"Tumetumia Udongo, miamba ambapo hivi vyote vinapatikana katika maeneo yetu yanayoondoa madini hayo na yakipita katika miamba na madini hayo yanakuwa hayana kemikali ambazo zinaongezwa wakati wa uchujaji maji." 

Amesema udongo na miamba hiyo inapatikana katika maeneo tofauti hapa nchini kama Lushoto Tanga pamoja na Kilimanjaro.

No comments :

Post a Comment