Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt. Ellen Senkoro akizungumza na
na baadhi wataalamu wa afya waliopata ajira ya muda kupitia taasisi ya
Benjamin Mkapa.
Mkurugenzi
Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru akizungumza
na na baadhi wataalamu wa afya waliopata ajira ya muda kupitia taasisi
ya Benjamin Mkapa
Katibu
Mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na menejiment ya Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Taasisi ya Benjamin Mkapa pamoja na baadhi ya viongozi wa
Wizara ya Afya
Baadhi wataalamu wa afya waliopata ajira ya muda kupitia taasisi ya Benjamin Mkapa wakiwa kwenye picha ya pamoja na katibu mkuu.
TAASISI
ya Benjamin Mkapa (BMF) kupitia ufadhili wa mashirika ya Maendeleo ya
Irish Aid, UKAID-DFID na UNFPA, imeajiri watumishi wa kada mbalimbali
za afya 575 kwa muda wa miezi sita kuanzia mwezi Julai 2020 wtakaofanya
kazi katika Halmashauri 72 zilizopo kwenye mikoa mitatu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ajira hizo leo Julai 8,2020 Katibu Mkuu Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchemba
amewaasa wote watakaoajiriwa kupitia mradi huo wa BMF kufanya kazi kwa
kufuata taratibu za kitaalamu huku Pia akiwasishi kuzingatia maadili ya
utumishi na kujitahidi kuwa mfano katika maeneo watakayokuwa wakifanya
kazi.
"Uadilifu
wenu katika utoaji wa huduma ni wa muhimu kwani mtakuwa ni kioo cha
namna sekta yetu ya Afya inavyofanya kazi", amesema Prof. Mchembe.
Amesema, ajira hizo wanazoingia na Taasisi ya BMF ni ajira za muda wa miezi sita.
"Mmepangwa kufanya kazi katika maeneo yaliyopewa kipaumbele chini ya mikoa 13 iliyopo hapa Tanzania bara.
Maeneo
mliyopangwa ni yale ambayo Serikali imeona ni vyema kuongeza nguvu
katika kuimarisha huduma za Kinga na Tiba dhidi ya maradhi mbali mbali
mfano UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu, Magonjwa ya Mlipuko mfano
Corona
n.k pamoja na kuimarisha huduma ya Afya ya Uzazi... wote mliochaguliwa
mmepewa kipaumbele hicho kwa kuwa mlikuwa mnajitolea
katika
maeneo mliyopangwa hivyo basi, Serikali ikaona ni vyema kuwatumia
katika mfumo rasmi kwa kipindi cha miezi sita", amesema Prof. Mchembe
Jumla
ya Halmashauri 72 zilizopo katika mikoa 13 imepewa kipaumbele ikiwemo
Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Mara, Pwani, Dodoma, Arusha, Mtwara,
Kigoma, Mwanza, Simiyu, Mbeya na Songwe. Mbali na mikoa hiyo 13 ya
Tanzania bara, pia mradi utawezesha upangaji wa watumishi 21 kwa upande
wa Tanzania Visiwani ambapo huo mchakato wake unaendelea ili kuweza
kuzingatia taratibu za ajira za Tanzania Visiwani.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt.
Ellen Senkoro amesema kuwa Tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Mkapa
takriban miaka 14 iliyopita, taasisi imeendelea kushirikiana na
serikali, katika jitihada zake za kuhakikisha utoaji wa huduma bora za
afya kwa wananchi ikiwemo pia kupatia ufumbuzi wa kupunguza upungufu wa
wataalamu wa afya, ambao mpaka sasa umekadiriwa kuwa ni wa asilimia 52
ya watumishi wote wanaohitajika hapa nchini.
Amesema,
watumishi hao 575 wanatoka katika fani 13 ambazo ni Mteknolojia
Maabara Mteknolojia Maabara Msaidizi, Tabibu ,Tabibu Msaidizi, Daktari
II, Afisa Muuguzi Msaidizi, Afisa Muuguzi Afisa Ustawi wa Jamii , Afisa
Ustawi wa Jamii Msaidizi , Mteknolojia Dawa , Mteknolojia Maabara
Msaidizi , Afisa Afya Mazingira, na Afisa Afya Mazingira Msaidizi.
Aidha
Dkt, Senkoro ameshukuru Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI kwa
ushirikiano wao madhubuti na mkubwa sana walioutoa katika kufanikisha
ajira hizo.
Naye,
Katibu Mkuu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof.
Lawrence Museru amesema, Muhimbili inayo furaha kufanya kazi na Taasisi
ya BMF ana kwamba watumishi 575 watakaopata ajira hizo, watumishi 80
wamepangiwa kufanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
No comments :
Post a Comment