Thursday, July 16, 2020

MEMBE AFUNGUKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, ATAJA VIPAUMBELE ACT IKICHUKUA NCHI


ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Awamu ya Nne Bernard Membe amejiunga rasmi Chama cha ACT Wazalendo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwamba katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu njia ya kwenda Ikulu ni nyeupe kwa Chama hicho.
 
Na Mwandishi Wetu, TV

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Awamu ya Nne Bernard Membe amejiunga rasmi Chama cha ACT Wazalendo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwamba katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu njia ya kwenda Ikulu ni nyeupe kwa Chama hicho.

Membe amesema hayo leo Julai 16,2020 katika Ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa kwa wanachama wa ACT Wazalendo ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa  amejiunga  na chamaa hicho ili kuleta mabadiliko ya kweli.

"ACT Wazalendo ni chama ambacho kinakuwa kwa kasi sana kuliko vyama vingine vya upinzani.Nimesoma katiba ya ACT na kujiridhisha ndicho chama sahihi cha mimi kutoa mchango wangu  kupitia chama chenye usawa,haki na kuheshimiana ambayo ni baadhi ya mambo  yanayomvutia.

"Nilifukuzwa na CCM kwa msimamo wangu  wa kuikosoa serikali pamoja na nia yangu ya  kutangaza kugombea urais 2020 zimesababisha nifukuzwe.Nimekuja ACT kwa sababu ni Chama makini kinataka mbaadiliko na huu ni mwaka wa kuchukua dola.ACT ni chama ambacho kimejipambanua kutetea haki na usawa kwa watu wote,"amesema Membe.

Akifafanua  kuhusu yeye kujiunga na Chama hicho amesema ni kutokana na demokrasia ya kweli iliyopo na kubwa  zaidi wamekuwa watetezi wa watu ambao wanaonewa."Watu ambao wanamsikiliza wanajua nipo kwenye chama ambacho kikisema kinatenda."

Kuhusu uchaguzi mkuu Membe amesema wakipata ridhaa ya kwenda Magogoni(Ikulu) watashughulikia ajira za vijana kwani wengi wao wako mtaani kwa kutokuwa na ajira.

Pia amesema wakishika  Dola wataangalia suala la mishahara ya watumishi mbalimbali kwani lazima iongezwe."Mshara mara ya mwisho iliongezwa mwaka 2015. Hivyo ACT tukifanikiwa tutaongeza mishahara ya watumishi wote.

"Katika utawala wa ACT Wazalendo hakutakuwa na vitisho wala hofu ya aina yoyote.Pia tutahakikisha wawekezaji wanapata fursa na kuwekeza. Muwekezaji sio adui, wanatakiwa kuwa marafiki wa serikali iliyoko madarakani, ACT  itawatafuta na kuwarejesha wawekezaji na wafanyabiashara nchini. Hakuna sababu ya kuwakomoa, kuwasumbua na kuwatumbua.Kodi zao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi .Wawekezaji ni kama ndege ukimfukuza anakwenda kwingine,"amesema Membe

Pia amesema iwapo ACT Wazalendo itapata ridhaa ya kushika dola itahakikisha inarudisha uhusiano wa kidiplomasia kati yake ya nchi nyingine. Serikali yao itaheshimu utawala wa sheria na itaanzisha mchakato wa Katiba."Nchi yoyote inayoheshimika duniani lazima iongozwe kwa misingi ya Katiba na Sheria".

Membe amefafanua kwamba walitarajia mchakato wa Katiba Mpya ambao ulianzishwa na Serikali ya Awamu ya Nne ungeendelea  lakini Serikali ya Awamu ya Tano imeshindwa kuendeleza.

Ameeleza kuwa kuna miradi ambayo kwa sasa haiendelezwi licha ya huko nyuma kuwa ilishaanza kutekelezwa akitolea mfano wa mradi wa bandari ya  Bagamoyo ambao mchakato wake ulianza na sasa haupo tena."ACT Wazalendo ikiingia madarakani itahakikisha inarudisha mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

"Pia mradi wa gesi ambao umesimama unastahili kuendelezwa.Watu wa Lindi na Mtwara wameumia sana, wameteseka, kila kunapokuwa na kitu cha kuwanyanyua kinabwaga. Lazma wananchi wa Lindi na Mtwara na mikoa.mingine wasaidiwe kuinuliwa kiuchumi,"amesema Membe.

No comments :

Post a Comment