Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga alipotembelea banda la NHIF
na kujionea huduma zilizotolewa katika maonesho ya sabasaba
Picha mbalimbali za utoaji huduma katika banda la NHIF katika maonesho ya Sabasaba.
Na Mwandishi Wetu
JUMLA
ya wanachama wapya 1,500 wamejiunga na huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) katika maonesho ya Sabasaba yaliyoanza tangu Julai 1,
mwaka huu.
Wanachama
hao wamejiunga kupitia utaratibu wa Vifurushi vipya ambavyo ni vya
Najali, Wekeza na Timiza pamoja na mpango wa watoto chini ya umri wa
miaka 18.
Mbali na wanachama hao wapya, zaidi ya wananchi 2,500 wameelimishwa juu ya umuhimu wa huduma za bima ya afya Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kwamba, kitendo cha Mfuko
kuweka na kuwezesha wananchi wote kuchagua huduma wanazotaka kujiunga
nazo kumesaidia kwa kiwango kikubwa kurahisisha utaratibu wa kujiunga.
“Tunashukuru
Mfuko kwa kushiriki maonesho haya na kutoa huduma za usajili ambazo
zimeturahisishia sisi kufika hapa na kujiunga moja kwa moja, huduma za
matibabu ni za msingi ambazo zinaleta ujasiri mkubwa ndani ya familia,”
Walisema wananchi.
Akizungumza
katika maonesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alitoa
wito kwa wananchi kutumia fursa za maonesho na mikusanyiko mingine kwa
ajili ya kupata huduma za Bima ya Afya ili kujihakikishia huduma za
matibabu.
“Nimefarijika
sana hapa kuona wananchi wameamua kujiunga na huduma zetu na
kujihakikishia huduma za matibabu na kwa sasa hakuna tena sababu za
kushindwa kujiunga kama ilivyokuwa awali, tumeweka utaratibu rahisi sana
wa kujiunga unaomwezesha kila mmoja kujiunga na kupata huduma,” alisema
Konga.
Alisema
kuwa Mfuko umejipanga kupitia ofisi zake zote zilizoko mikoa yote
Tanzania kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwafikia katika maeneo yao
kuwapa elimu na kuwahamasisha ili wajiunge na huduma.
“Niwahakikishie
tu wananchi kuwa Mfuko umejipanga sana kuhakikisha unatoa huduma bora
na za haraka kwa wanachama wake na katika kipindi hiki ambacho nchi yetu
imeingia kwenye Uchumi wa Kati ni vyema kila mwananchi akawa na uhakika
wa kupata huduma za matibabu ili tuweze kuzalisha na kuongeza vipato
vya kaya na Taifa kwa ujumla,” alisema Konga.
No comments :
Post a Comment