Na.Mwandishi
Wetu-MAELEZO
Serikali
imesema inatarajia kugharamia Elimu ya Juu kwa wanafunzi wapya 50,000 kwa mwaka wa masomo 2020/2021
ili kuwezesha watoto wanaomaliza kidogo cha sita ambao wanakipato cha chini
kumudu mahitaji ya kupata eimu ya juu.
Akizungumza
katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq
Badru alisema kuwa Maonesho ya Biashara (DITF) ni maandalizi ya kuanza msimu
mpya wa kufungua maombi ya Mikopo kwa wananfunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa
masomo 2020/21.
“Sisi
Maonesho haya yanatusaidia sana kwa sababu huwa ni maandalizi ya kuanza msimu
mpya na tuko tayari kufungua msimu huo kwa mwaka wa masomo 2020/21, bajeti mpya
ya serikali iliyopitishwa bungeni ya Bilioni 468 hii itatuwezesha kulipia
wanafunzi wapya wasiopungua 50,000”, Alisema Badru
alibainisha
kuwa kwa mwaka huu wa masomo unaoanza novemba kutakuwa na wanafunzi wapya
wanaofaidika na mkopo wa elimu ya juu wapatao 50, 000 na kufanya idadi ya
wanafunzi wanaolipiwa na Bodi hiyo kuwa 225,000 ambapo wote watakuwa
wanafaidika na bajeti mpya ya bilioni 468.
Aliongeza
kuwa katika mwaka wa masomo 2019/20 wanafunzi wapya walikuwa 45,000 ambapo
bajeti ilikuwa bilioni 450 kwa wanafunzi wote wapya na wanaendelea na mwaka huu wa masomo yaani 2020/21 kutakuwa
na wanafunzi 50,000 ambapo shilingi bilioni 468 imepitishwa ili kugharamia
masomo kwawanafunzi wote.
Aidha
alieleza kuwa bajeti imekuwa ikiongezeka kila mara kwa muda wa miaka minne na
sasa Bodi hiyo imewekeza jumla ya TZS Trilioni 2.6 kuwasomesha wanafunzi tokea
mwaka 2015, huku ukusanyaji wa mikopo iliyoiva ukiongezeka kutoka Bilioni 30 mwaka
2014/15 na kufikia bilioni 192 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka huu.
No comments :
Post a Comment