Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi
(wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo moja ya kitanda kati ya vitano na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kata ya Iyumbu mkoani
Singida jana. Kutoka kulia ni Meneja Mahusiano wa Kanda Biashara na
Serikali wa benki hiyo, Peter Masawe, Meneja wa benki hiyo, Wilaya ya
Ikungi, Osward Kayuni na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Katalyeba Vitalis.
Wananchi wa Kata ya Iyumbu wakiwa kwenye hafla ya kupokea vifaa hivyo.
Wananchi wa Kata ya Iyumbu wakiwa kwenye hafla ya kupokea vifaa hivyo.
Wananchi wa Kata ya Iyumbu wakiwa kwenye hafla ya kupokea vifaa hivyo.
Watumishi wa Idara ya Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Meneja wa benki hiyo, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni akizungumza katika hafla hiyo.
Wananchi wa Kata ya Iyumbu wakiwa kwenye hafla ya kupokea vifaa hivyo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Katalyeba Vitalis, akisoma taarifa fupi ya kituo hicho cha afya.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akihutubia katika hafla. Kutoka kulia ni Meneja Mahusiano wa Kanda Biashara na Serikali wa benki hiyo, Peter Masawe, Meneja wa benki hiyo, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo moja ya vitanda hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akikabidhiwa madawati.
Vitanda vikikabidhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akimfunika shuka mkazi wa kata hiyo Flora Paul ambaye alikuwa akizindua moja ya vitanda kwa staili ya kulala.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo. |
Afisa Elimu wa Kata ya Ntuntu, Kitila Mkumbo akitoa shukurani baada ya kupewa msaada wa madawati.
Mkazi wa kata hiyo, Flora Paul akishukuru baada ya kupokea msaada huo.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa Kata ya Iyumbu, Wilikista Ochien’g, akishukuru.
Mkazi wa kata hiyo, Mpinya Shaha, akishukuru baada ya kupokea msaada huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MKUU
wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo amewataka wajawazito
katika Kata ya Iyumbu wilayani humo kujenga tabia ya kuhudhuria kliniki
baada ya kusogezewa kituo cha afya.
Mpogolo
alitoa ombi hilo jana wakati akipokea vifaa tiba vyenye thamani ya
sh.milioni 5 vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya Kituo cha Afya
cha Kata ya Iyumbu.
“Wakina
mama sasa mmesogezewa huduma za afya na leo Benki ya NMB imewaletea
msaada wa vifaa tiba jengeni mazoea ya kwenda kliniki ili kufanyiwa
uchunguzi wa afya zenu mnapokuwa wajawazito” alisema Mpogolo.
Alisema
hapa nchini kuna benki zaidi ya 49 zikiwepo na ndani ya Mkoa wa Singida
lakini ni benki ya NMB pekee ndio imeonesha upendo na kuwa pamoja nao
kwa kuwapelekea vifaa tiba hivyo.
Mpogolo
alisema benki hiyo sio kwamba wana fedha nyingi la hasha lakini
imewapelekea msaada huo pamoja na madawati ya kukalia wanafunzi wa Shule
ya Msingi Ntuntu yenye thamani ya sh.milioni 5 jumla ikiwa ni
sh.milioni 10.
Alisema
benki hiyo hata katika kipindi cha ugonjwa wa Covid 19 ilitoa msaada na
pia Serikali ilipotaka gawio kwa ajili ya shughuli za maendeleo ilitoa
zaidi ya sh.bilioni 10.
“Niishukuru
sana Benki ya NMB kwa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wetu Dkt.John
Magufuli za kuwaletea maendeleo wananchi” alisema Mpogolo.
Alisema
mwanadamu akiwa na afya njema anaweza kushiriki shughuli mbalimbali za
maendeleo na ndio maana benki hiyo imeliona hilo na kuwapelekea msaada
huo.
Aidha
Mpogolo alisema katika kipindi kifupi ambacho Rais Magufuli amekuwa
madarakani ameweza kujenga zaidi ya Hospitali 67, Vituo vya Afya na
Zahanati zaidi ya 400 na kwa Wilaya ya Ikungi wamepata vituo vya afya
viwili cha Kata ya Ihanja kilichojengwa kwa sh.milioni 500 pamoja na
vifaa tiba vya zaidi ya sh.milioni 300 na kituo cha afya cha Kata ya
Sepuka cha sh.milioni 400 pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi
ya milioni 200.
Mpogolo
alitumia nafasi hiyo kuuomba uongozi wa benki hiyo kufungua tawi katika
kata hiyo ambayo ndio chanzo kikubwa cha mapato ya wilaya hiyo ili
kuwasaidia wananchi kuweza kuweka fedha zao badala ya kwenda makao makuu
ya wilaya hiyo au Singida mjini ambako kuna umbali wa kilometa zaidi
165 na wanapo kuwa njiani kwenda kuziweka wanakuwa na wasiwasi wa
usalama wao na fedha zao.
Meneja
wa benki hiyo Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi akikabidhi msaada huo alisema
benki hiyo wakati wote imekuwa ikisaidia shughuli za maendeleo hapa
nchini ikiwa ni kuunga jitihada za Rais Magufuli za kuiletea nchi
maendeleo.
Alisema
benki hiyo ina matawi zaidi ya 230 nchi nzima lakini katika Kanda ya
Kati wanamatawi takribani 25 ambapo alimwagiza meneja wa benki hiyo
Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni kuhakikisha anapata wakala katika kata
hiyo ya Iyumbu ili kuwapunguzia wananchi changamoto ya kutunza fedha
zao.
Mlozi
alitaja vitu walivyotoa msaada katika kata hiyo mbali ya vitanda
vitano; vitatu vikiwa vya kawaida na viwili vya kujifungulia, vifaa tiba
seti moja vya kujifungulia, magodoro na madawati pia walitoa mashuka
18 vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 10.
Mlozi alisema benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuchagiza maendeleo mbalimbali hapa nchini.
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Katalyeba Vitalis alisema kituo hicho cha
afya kimeanza kutoa huduma rasmi Julai 20 mwaka huu kwa wakazi zaidi ya
11,000 wa kata hiyo ambao wanatoka katika vijiji vitatu.
Alisema
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupitia Mkurugenzi wake Justice Kijazi
ilitoa sh.milioni 1.5 kwa ajili ya kukarabati jengo la muda la kukodi
lengo likiwa ni kupanua wigo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi wa
Kata ya Iyumbu iliyopo pembezoni mwa wilaya hiyo ambao walikuwa
wakitembea umbali mrefu hadi Mgungila na Singida mjini kufuata huduma za
afya.
Alisema
halmashauri hiyo imetoa jumla ya sh.milioni 4 kwa ajili ya kulipia
jengo hilo la kukodi na kuwalipia pango watumishi watatu wa kituo hicho.
Alisema
kituo hicho ni cha muda kwani wanatarajia kupata sh.milioni 500 kutoka
Serikalini kwa ajili ya kujenga kituo cha afya cha kudumu.
Meneja wa benki hiyo, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni aliwaomba wananchi na wafanyabiashara katika kata hiyo na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi kufungua akaunti kwenye benki hiyo kubwa hapa nchini ambayo huduma zake zimesogezwa jirani na wananchi.
Meneja wa benki hiyo, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni aliwaomba wananchi na wafanyabiashara katika kata hiyo na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi kufungua akaunti kwenye benki hiyo kubwa hapa nchini ambayo huduma zake zimesogezwa jirani na wananchi.
Wananchi
wa Kata hiyo Mpinya Shaha, Flora Paul na Wilikista Ochien’g
waliishukuru Serikali na benki hiyo kwa kuwapelekea kituo hicho cha afya
na msaada huo.
No comments :
Post a Comment