Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Hussein Mwinyi ametoa shukrani kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho pamoja na wanaCCM wote kwa kupitisha jina lake kugombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Akizungumza baada ya jina lake kupitishwa na mkutano huo leo Julai 10, 2020 baada ya kupata kura 129 sawa na asilimia 78 ya kura zote zilizopigwa, Dk.Mwinyi amesema kuwa kwanza kabisa anachukua nafasi hiyo kumshukuru Mungu na leo mchakato huo umekamilika kwa amani na salama."Namshukuru hatimaye leo hii tumefikia hatua hii kwa amani na usalama."
"Namshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli kwa kutufiksha hapa tukiwa salamam namshukuru Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuusimamia mchakato huu tangu hatua za mwanzo kule Zanzibara, wagombewa walikuwa 32 katika Kamati Maalum wamepatikana watano na nini nikiwemo, nashukuru kwa hatua ile Kamati Kuu jana imetoa wagombea watatu na leo nimepatikana mimi kama mpeperusha bendera.
"Hii ni heshima kubwa , kura 129 ni nyingi sana, nataka niwaahidi nitafanya kazi ya kulitumikia Taifa hili kwa uwezo wangu wote, kinachonipa faraja pamoja na kwamba tulikuwa 32 lakini wenzangu wote wameahidi kushirikiana nami, kwa sasa tuna timu moja tu ya CCM,"amesema Dk.Mwinyi mbele ya wajumbe wa mkutano huo uliopitisha jina lake.
Amesisitiza kuwa faraja kubwa anayoipata timu hiyo imekuwa moja na wajumbe wote wa mkutano mkuu, viongozi wa mashina na matawi anajua watakuwa pamoja katika kutafuta ushindi, na kwamba atakuwa tayari kufanya kazi na wote."Ahadi yangu kwenu ni kama mlivyosema ninyi tunakwenda kutafuta ushindi. Nawashukuru nyote, kwenye maisha yangu nimefanya mitihani mingi lakini mtihani mkubwa ulikuwa huu.
"Lakini namshukuru leo tumemaliza huku nikujua kazi iliyoko mbele ni kubwa lakini uzuri siyi yangu pekeyangu, nawashukuru wote mlionipigia kura, pia nawashukuru na wale wote ambao hamkunipigia kura,"amesema Dk.Mwinyi huku akishangiliwa na wajumbe wa HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi .
No comments :
Post a Comment