Afisa masoko kutoka TAMWA-ZNZ
Muhidini Ramadhani akigawa mbegu za mchicha na pilipili kwa
wajasiriamali kutoka Shehia ya Kiboje Unguja kwa lengo la kuwawezesha
wajasirimali hao kiuchumi.
Afisa masoko kutoka TAMWA-ZNZ Muhidini Ramadhani akiwasomea
mkataba wa makabidhiano ya vifaa wajasiriamali wa shehia ya Mtende
Makunduchi mkoa wa kusini Unguja kabla ya kuwakabidhi rasmi vifaa mbali
mbali ambavyo vitatumika kwa ajili ya uzalishaji mali.
Afisa Masoko kutoka TAMWA-ZNZ
Muhidini Ramadhani akisisitiza jambo wakati alipokua akizungumza na
wajasiriamali wa Shehia ya Kidutani Unguja mara baada ya kuwakabidhi
msaada wa vifaa mbali mbali.
***************************
Na Masanja Mabula , Zanzibar.
JUMLA ya Shilingi Milioni saba
zimetumika na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ kwa ajili
ya ununuzi wa vifaa mbali mbali vya kuwawezesha wajasiriamali
katika
maeneo tofauti Unguja na Pemba huku lengo kuu likiwa ni kuwakuza
wajasiriamali hao kiuchumi.
Msaada huo umekuja siku chache
baada ya kufanyika kwa ziara ya Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt,Mzuri Issa
katika vikundi hivyo ili kujionea shughuli za uzalishaji pamoja na
changamoto.
Akitoa taarifa kuhusu vifaa hivyo
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema msaada huo umehusiaha
vifaa tofauti kama vile vifaa vya kuwezesha wajasiriamali zao kutengeza
sabuni pamoja na kuwawezesha katika shughuli za kilimo.
Alisema wiki moja iliopita baada
ya kufanya ziara katika maeneo yote ambayo Chama hicho kinawezesha
wajasiriamali hao walipata maombi ya wahusika na kuona ni vyema
kuyafanyika kazi.
Alisema kwa kuwa zipo jitihada kubwa zinazoendelea kufanya wakaona ipo haja ya kuwaunga mkono ikiwemo pamoja na kuwapatia vifaa.
Akitoa ufafanuzi wa vikundi
ambavyo vitafaidika na msaada huo kwa upande wa Unguja alisema ni
vikundi 12 na kwa Pemba ni 24 vikundi ambavyo vyote vimeanzishwa miezi
mitatu iliopita chini ya usimamizi wa TAMWA-ZNZ.
Awali afisa masoko kotoka
TAMWA-ZNZ Muhidini Ramadhani aliwataka wajasiriamali hao kuwa makini
sambamba na kuhakikisha utunzaji wa vifaa hivyo kwa muda wote.
Alieleza kuwa iwapo vifaa hivyo
vitatumika ipasavyo vitaweza kuleta tija kubwa ikiwemo kusaidia
maendeleo kwa wananchi hao na Taifa kwa ujumla.
Lakini pia Afisa huyo alieleza
kuwa Zanzibar kwa sasa kuna fursa nyingi ikiwemo za matunda na mboga
mboga hivyo kuna kila sababu wajasiriamali hao kuzitumia.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya
wanjasiriamali hao kutoka mkoa wa kusini Unguja walieleza kufuurahishwa
kwao na hatua hio muhimu iliofanywa na TAMWA-ZNZ na kwamba wanaahidi
vifa hivyo wataendelea kuvitunza ili viweze kuleta tija kwao.
Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mbegu za mboga mboga,keni za maji na trea zinazotumika kuzalisha sabuni
No comments :
Post a Comment