Benki
ya wakulima (TADB) ikiongozwa na Mkurgenzi Mtendaji, Japhet Justine,
wameshiriki katika ufunguzi wa msimu mpya wa kahawa 2020/21
uliofunguliwa na RC Kagera Mh. Brig. Gaguti wilayani Kyerwa jana
Jumanne.
‘TADB
inaendelea kuwa mdau mkuu wa wakulima tangu msimu 2018/19 tulipoanza
kwa kuwekeza bil 30 na bil 23 kwa msimu 2019/20 na kutokana na kufanya
vizuri, Oct 2019 tuliwatembelea na kutunuku pikipiki kwa vyama vya
Luicho na Nyakatuntu’ amesema Mkurugenzi Mtendaji Japhet Justine
Amesema
TADB imeleta mapinduzi kwa wakulima 142,000 na kuendelea kuhamasisha
wakulima kujiunga na vyama na kufungua benki akaunti na mpaka sasa
wanalipwa kupitia benki
Amesisitiza
kwamba kwa vile Serikali ya awamu ya 5 inahimiza na kudhamiria
maendeleo ya moja kwa moja kwa wakulima wadogo, hivi sasa TADB imeshusha
riba kutoka 12% hadi 9% yote hayo kutokana na uaminifu wenu na punguzo
hili litapunguza gharama na kuongeza tija kwa wakulima
"Wakati
tunaanza vyama vilikuwa na madeni makubwa hadi bil 7, mpaka sasa KDCU
hawana deni na KCU wanamalizia. Hivyo tungependa vyama visimame na
vijiendeleze vyenyewe kwa ufanisi. Tunahitaji kuviwezesha vyama hivi kwa
maendeleo ya uchumi wa wakulima", aliongeza Mkurugenzi Mtendaji wa TADB
Mkoa
wa kagera unazalisha 68% ya ndizi nchini, na kahawa 45% ilitoka Kagera
na tulikusanya kilo million 52 na kuzalisha billion 84, ikiwa malengo ya
msimu huu ni kukusanya kilo million 60. Tunajivunia kwamba mwaka huu
hakukuwa na changamoto kama miaka mingine, kulikuwa na utulivu hivyo
tunaomba wakulima waendele kufata kanuni bora za kilimo pamoja na
kutumia mizani ya kidijitali. Asisitiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Aidha,
Bw. Oscar, Meneja KDCU amesema msimu mpya wa 2020/21 vyama vitanunua
kahawa kwa wakulima kiasi cha shilingi 1200/- kwa kilo ikiwa ni
ongezeko kutoka 1100 msimu uliopita. Bei hii ina tija kwa wakulima kwani
soko la dunia bei ni sh. 850 hadi 867, Asante sana TADB kwa kuwezesha
hili.
No comments :
Post a Comment