Wednesday, June 3, 2020

Stendi ya mabasi, kituo cha malori Dodoma kuanza kutumika

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge Na Joyce Kasiki, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amtangaza kuanza kutumika kwa Soko Kuu la
Ndugai, Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoano na Kituo cha malori Nala jijini hapa ifikapo Juni 8,mwaka huu.
Akizungumza wakati akiikabidhiwa miradi hiyo baada ya kukamilika jijini hapa leo, Dkt. Mahenge ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa kujenga miradi hiyo ambayo imezidi kupandisha hadhi ya Jiji la Dodoma.
“Kuanzia Juni 8, mwaka huu mabasi yote yaendayo mikoani yahamie stendi mpya maana kituo kimeshakamilika na Terminal zote zilizokuwa zinatumika tunazipa muda wa siku 30 ili nao wahamie stendi mpya na terminal zao zitabaki na kazi ya kuhudumia magari yao tu.” Amesema Dkt.Mahenge.
Amesema malori yenye zaidi ya tani tatu yawe yamehamia kituo cha kupaki malori eneo la Nala ifikapo Juni 8 mwaka huu.

No comments :

Post a Comment