Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa
Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea
Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Nyangoma James
Mama mwenye Ulemavu wa miguu msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya
kununulia Bajaji ili imsaidie kuendesha Maisha yake. Pia Rais Dkt.
Magufuli aliendesha Mchango kwa Wananchi wengine ambapo waliahidi
kumchangia mama huyo kiasi cha Shilingi Milioni 3.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya
kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5. kushoto aliyekaa ni Mkuu wa
Wilaya ya Ubungo Kisare Makore.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama mwenye
Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha
Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa hamasa
pamoja na Wananchi wa Ubungo mara baada ya kuwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la
Ubungo Darajani mara baada ya kuzungumza na Wananchi.
PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………….

No comments :
Post a Comment