Rais
wa Tanzania, Dkt Magufuli ametangaza kumsamehe aliyekuwa Kamishna Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye baada ya kiongozi
huyo kumuomba msamaha mara kadhaa.
huyo kumuomba msamaha mara kadhaa.
Rais
ametangaza msamaha huo wakati akizindua jengo la jeshi hilo jijini
Dodoma, ambapo mbali na Andengenye ametangaza pia kuwasamehe maafisa
wengine wa jeshi hilo ambao wanatuhumiwa kuhusika kwenye ubadhirifu wa
fedha.
Januari
23 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Andengenye na aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kufuatia mkataba mbovu
ambao jeshi hilo liliingia na Kampuni ya Romania kwa ajili ya ununuzi wa
vifaa mbalimbali. Wakati huo huo aliridhia barua ya kujiuzulu ya
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Jacob
Kingu.
Jeshi
la Zimamoto lililiingia mkataba huo wenye thamani ya shilingi trilioni 1
bila kufuata sheria, kwani zabuni hiyo haikuwa imepangwa kwenye bajeti,
wala haikupitishwa na bunge.
Akizungumza
wakati akitangaza msamaha huo Rais alisema kwamba licha ya kwamba
amemsamehe, lakini hatomrejesha kwenye jeshi hilo, badala yake
atapangiwa kazi sehemu nyingine.
No comments :
Post a Comment