Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Venance Mabeyo akikagua paredi maalum la askari wapya kundi 39/20
waliohitimu mafunzo ya uaskari katika Chuo cha Mafunzo ya awali
RTS-Kihangaiko, Msata Mkoani Pwani.(Picha na Luteni Semunyu)
Baadhi ya Askari wapya wanawake
kundi 39/20 wakiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa waliovalishwa
Medali kwa kufanya vizuri wakati wa kufungwa mafunzo ya awali ya
kijeshi katika Chuo cha Mafunzo RTS-Kihangaiko, Mkoani Pwani.( Picha na
Luteni Selemani Semunyu)
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance
Mabeyo akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mafunzo ya
awali katika chuo cha mafunzo ya awali RTS-Kihangaiko Picha na Luteni
Selemani Semunyu.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance
Mabeyo akikata utepe kuzindua Mradi wa maji katika chuo cha mafunzo ya
awali RTS-Kihangaiko Picha na Luteni Selemani Semunyu.
******************************
Na Luteni Selemani Semunyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini
Jenerali Venance Mabeyo amepongeza chuo Cha mafunzo ya awali ya Kijeshi
cha RTS Kihangaiko kutokana na usisimamizi wa mafunzo na Ujenzi wa
Miradi ya kujitegemea.
Jenerali Mabeyo alisema hayo
mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe za kuapa kwa Askari wapya kundi la
39 katika chuo hicho kilichopo Msata Bagamoyo Mkoani Pwani.
“Sina Shaka na mazoezi mliopatiwa
na nimeshuhudia pia kupitiaa vyombo vya habari mlipokuwa mkihitoimisha
mafunzo ya Porini mnastahili pongezi” Alisema Jenerali mabeyo
Alisema kufanya zoezi la pamoja kwa kujumuisha vikosi mbalimbali tena kwa kutumia gharama za shule ni hatua kubwa ya kupongezwa.
Aliongeza kuwa anafurahi kuona
Askari wapya mbele yake kwani ni ishara kwamba wameiva wako imara katika
kutumikia JWTZ lakini pongezi kubwa ni kwa wakufunzi waliohakikisha
wanafika hatua hiyo.
Aidha aliwataka askari wapya
kuhakikisha wanalinda nchi kwa uadilifu kwani ndio jukumu lao kubwa na
kuwa waadilifu kwa kuishi kiapoa chao.
” Muhakikishe mnaishi kiapo chenu
na muwe tayari kutekeleza majukumu hayo mahala popote bila kuchagua
kwani jeshi ndio linajua wapi mnaweza kutumika, Alisema Jenerali Mabeyo.
katika hatua nyingine aliwataka
watu wote wenye jambo au masuala na jeshi hilo kutozunguka wafuate
utaratibu wa kijeshi badala kutaka kuwatumia viongozi wengine wakati
Mkuu wa majeshi na wasaidizi wake wapo.
” Usifikiri ukimueleza Rais shida
yako ukadhani haitorudi kwetu au ukimweleza Waziri au ukinieleza mimi
ndio litashughulikiwa haraka tufuate utaratibu, Alisema Jenerali Mabeyo.
Kuhusu Miradi alisema ipo haja ya
jeshi la wananchi kuendelea kuweka jitihada katika miradi yao wenyewe
ili kuepusha adha mbalimbali na matumizi yasiyo ya lazima.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa
shule ya mafunzo ya awali RTS Kihangaiko Kanali Sijaona Myala alisema
askari waliohitimu ni 3575 wanaume wakiwa 3245 na wanawake ni 330 huku
11 wakipoteza maisha wakati wa Mafunzo.
Aliongeza kuwa wamejifunza mambo
mbalimbali kulingana na silabi ya mafunzo huku akisema mambo manne
muhimu wanayotakiwa kuyafanya wawapo jeshini muda wote ni utii,
uaminifu, na Uhodari.
“Mna dhamana kubwa sana ndani ya
jeshi, dhamana hii mkaitumie vizuri, jiepusheni na migogoro baina yenu
na raia ikiwa ni pamoja na kujichukulia hatua mikononi” Alisema kanali
Myala.
Awali mkuu wa kamandi ya Vikosi
Chini ya makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Sharif Othman alisema
ameshuhudia uimaraa wao na ana matumaini makubwa na Askari hao.
No comments :
Post a Comment