Mgodi wa
Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya
Twiga Minerals Corporation umetoa msaada wa vifaa wezeshi kwa watu
wenye ulemavu na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa wazee katika kata
ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 8.
Hafla
fupi ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika leo Jumatano Juni 24,2020
katika kijiji cha Bunango kata ya Bugarama ambapo mgeni rasmi alikuwa
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha.
Kaimu
Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena
Senkondo amevitaja vifaa vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
kuwa ni Fimbo nyeupe 5 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa macho,magongo 5
na baiskeli 8 kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa miguu pamoja na kadi
450 za msamaha wa matibabu kwa wazee.
Alisema
kutolewa kwa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo
ya jamii (Corporate social responsibility -CSR) unaotekelezwa na Mgodi
wa Barrick Bulyanhulu ambapo walikubaliana na Halmashauri ya wilaya ya
Msalala kwamba asilimia 10 ya fedha ya CSR kwa ajili ya makundi maalumu
vikiwemo vikundi vya akina mama,vijana,wazee na watu wenye ulemavu.
“Vifaa
wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee tulivyotoa vina thamani ya
shilingi 8,050,000/= . Tunatoa shukrani kwa ushirikiano mzuri na
viongozi wa ngazi zote katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya
jamii hususani katika kuhudumia makundi maalumu.Tunaomba tuendelee
kushirikiana kwa ajili ya kujenga jamii kwa maendeleo
endelevu”,ameongeza Senkondo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa walengwa, Mkuu wa wilaya ya Kahama
Mhe. Anamringi Macha ameupongeza na kuushukuru Mgodi wa Barrick
Bulyanhulu kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa wezeshi kwa wazee na
watu wenye ulemavu katika kata za Bugarama na Bulyanhulu.
“Mgodi wa
Barrick Bulyanhulu mmekuwa sehemu ya familia ya wakazi wa halmashauri
ya wilaya ya Msalala kutokana na ushirikiano ambao mmekuwa mkiutoa kwa
jamii. Tunawashukuru kwa kuona umuhimu wa kuyafikia makundi maalumu
ambayo kimsingi yanashiriki katika shughuli za maendeleo katika
jamii”,amesema Macha.
“Serikali
itaendelea kushirikiana na mgodi wa Bulyanhulu na Taasisi mbalimbali
katika kuyahudumia makundi maalumu kwani serikali inaamini kuwa binadamu
wote ni sawa bila kujali huyu ana ulemavu au mzee.Tutaendelea
kuhakikisha watu wote wanaishi kwa amani”,ameeleza.
Mkuu huyo
wa wilaya amesema vifaa hivyo wezeshi (baiskeli,fimbo nyeupe na
magongo) vitawasaidia watu wenye ulemavu kuwapunguzia adha ambayo
wamekuwa wakiipata katika utekelezaji wa shughuli zao za kijamii na
kwamba kadi za msamaha wa matibabu zitawasaidia wazee hao 450 kupata
huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya pindi
wanapohitaji huduma za matibabu.
“Naomba
mkavitunze na mvitumie vizuri hivi vifaa. Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya hakikisha katika vituo vya afya,zahanati kuna madirisha kwa ajili
ya wazee na kama hakuna hayo madirisha basi hakikisheni wazee wanapewa
kipaumbele na kupewa dawa na kila mmoja anayefika hospitali akaona kuna
mzee awape nafasi kwanza wazee”,ameongeza Macha.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa
Kilagwire Amesema mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na halmashauri
hiyo wamekuwa wakitekeleza mpango wa uwajibikaji kwa jamiiinayozunguka
eneo la mgodi katika kata za Bugarama na Bulyanhulu ili kukuza na
kuimarisha ustawi wa makundi mbalimbali ya kijamii yaliyopo katika
maeneo hayo.
“Katika
utekelezaji wa Programu hii ya CSR kwa mwaka 2019/2020 kwenye afua ya
vijana,wazee na watu wenye ulemavu,uongozi wa kata husika uliweka
vipaumbele kwenye bajeti kusaidia makundi ya wazee na walemavu vyenye
jumla ya shilingi 20,000,000/= inayotolewa na mgodi wa Barrick
Bulyanhulu”,amefafanua.
Kwa
upande wao, Salome Samweli, Abbas Salum na Praygod Museveni wameushukuru
mgodi wa Bulyanhulu kwa kuwapatia watu wenye ulemavu baiskeli,fimbo
nyeupe,magongo na kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi
huo na wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika
jamii.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza kwenye hafla fupi
ya kukabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata
ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals
Corporation leo Jumatano Juni 24, 2020 katika kijiji cha Bunango kata ya
Bugarama halmashauri ya wilaya ya Msalala. wa Pili kulia ni Kaimu
Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena
Senkondo akifuatiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Bunango,kata ya Bugarama
,Anna Peter na Afisa Maendeleo kata ya Bulyanhulu, Anna Boniface. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Muonekano
wa vifaa wezeshi (baiskeli maalumu,fimbo nyeupe na magongo kwa ajili ya
watu wenye ulemavu katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya
wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vyote vyenye thamani ya shilingi
milioni 8 vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation
Muonekano
wa vifaa wezeshi fimbo nyeupe na magongo kwa ajili ya watu wenye
ulemavu katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation.
Muonekano wa kadi
450 za msamaha wa matibabu kwa wazee katika kata ya Bugarama na
Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini nchini ya Twiga Minerals Corporation.
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akielezea kuhusu vifaa
wezeshi kwa watu wenye ulemavu na kadi 450 za msamaha wa matibabu kwa
wazee katika kaya ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga vyenye thamani ya shilingi milioni 8
vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Bunango,kata ya Bugarama ,Anna Peter. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa Kilagwire akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Watu
wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bulyanhulu na Bugarama wakiwa
kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa wezeshi vilivyotolewa na Mgodi wa
Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe.
Anamringi Macha akizungumza wakati akiwakabidhi vifaa wezeshi kwa watu
wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu
vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. Mkuu huyo wa wilaya
aliwasihi watu wenye ulemavu kutunza vifaa hivyo (baiskeli,magongo na
fimbo nyeupe) ambavyo vitawasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe.
Anamringi Macha akisalimiana na watu wenye ulemavu wakati akiwakabidhi
vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na
Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe.
Anamringi Macha na viongozi mbalimbali wa kata ya Bulyanhulu na Bugarama
na halmashauri ya wilaya ya Msalala wakipiga picha ya kumbukumbu na
watu wenye ulemavu baada ya kuwakabidhi vifaa wezeshi (baiskeli).
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe.
Anamringi Macha na viongozi mbalimbali wa kata ya Bulyanhulu na Bugarama
na halmashauri ya wilaya ya Msalala wakipiga picha ya kumbukumbu na
watu wenye ulemavu baada ya kuwakabidhi vifaa wezeshi (magongo na fimbo
nyeupe).
Kaimu Meneja Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Senkondo akielezea kuhusu kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee 450 wanaoishi katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe.
Anamringi Macha akionesha sehemu ya kadi za msamaha wa matibabu kwa
wazee wanaoishi katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu halmashauri ya
wilaya ya Msalala vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi kadi ya msamaha wa matibabu mmoja wa wazee hao.
Wazee na Watu wenye ulemavu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Mzee
Praygod Museveni akiushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kutoa msaada wa
baiskeli,fimbo nyeupe,magongo kwa watu wenye ulemavu na kadi za msamaha
wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea
kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii.
Salome
Samwel akiushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kutoa msaada wa
baiskeli,fimbo nyeupe,magongo kwa watu wenye ulemavu na kadi za msamaha
wa matibabu kwa wazee na kuuomba mgodi huo na wadau wengine kuendelea
kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii.
Awali
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Dkt.Ntanwa
Kilagwire akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa wezeshi kwa
watu wenye ulemavu na wazee kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu
vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Afisa
Tarafa ya Msalala,Victoria Lusana akiushukuru Mgodi wa Barrick
Bulyanhulu kwa kuwapatia vifaa wezeshi watu wenye ulemavu na wazee
katika kata ya Bugarama na Bulyanhulu.
Afisa
Mawasiliano Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mary Lupamba akizungumza kwenye
hafla fupi ya kukabidhi vifaa wezeshi kwa watu wenye ulemavu na wazee
kutoka kata ya Bugarama na Bulyanhulu vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick
Bulyanhulu.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment