Monday, June 1, 2020

KATIBU MKUU BALOZI KANALI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TAIFA LA ISRAEL KWA TANZANIA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Taifa la Israel  kwa Tanzania Mhe. Oded Joseph ambaye analiwakilisha Taifa hilo kutokea Nairobi, Kenya. Kanali Balozi Ibuge katika mazungumzo hayo amweleza Balozi Oded, kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kukakabiliana  na kusambaa kwa COVID-19 na madhara sambamba na madhara cake.
Aidha, pamoja na mambo mengine Wawili hao katika mazungumzo yao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo ya kuendelea kukuza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na biashara baina ya Tanzania na Israel. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akifafanua jambo kwa Balozi wa Taifa la Israel nchini Mhe.Balozi Oded wakati wa mazungumzo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiagana na Balozi wa Taifa la Israel nchini Mhe.Balozi Oded  mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yao.

No comments :

Post a Comment