Katibu Mkuu
wa CHADEMA, John Mnyika
Na Penina Malundo, TimesMajira Online
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka Jeshi la
Polisi nchini kupanua wigo wa uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa
Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe usiku wa
kuamkia mapema leo jijini
Dodoma.
Kimesema uchunguzi huo utakaofanywa na Jeshi la Polisi unapaswa
kutosita kuchunguza mazingira ya kisiasa ya tukio hilo yaliyozunguka na
kauli zilizotolewa awali kabla ya kufanyika kwa shambulio hilo.
Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni,ameshambuliwa usiku wa kuamkia jana wakati akirejea nyumbani
kwake Area D jijini Dodoma.
Akizungumza leo waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu
wa CHADEMA, John Mnyika, amesema Mbowe anaendelea kupatiwa matibabu
katika hospitali ya DCMCT Ntyuka jijini humo Dodoma na kwamba chama
kimefikia uamuzi wa kadri ya ushauri wa madaktari watakaoendelea kuwapa
watafanya utaratibu wa kumsafirisha kuja Jijini Dar es Salaam ili kuweza
kupatiwa matibabu zaidi.
Amesema taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi leo imesema kuwa
tukio hili ni la kawaida na kwamba lisihusishwe na na masuala ya
kisiasa.
Mnyika amesema kwa sababu jeshi la polisi limesema linafanyia
uchunguzi, hivyo halipaswi kufunga uchunguzi na kuliita tukio hilo ni la
kawaida.
“Natoa wito kwa Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama
vilichunguze jambo hili kwa mapana na mawanda yake yote ili waliohusika
na tukio hili wafahamike kwa haraka na hatua za haraka ziweze
kuchukuliwa dhidi yao,”amesema Mnyika.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment