Shirika
la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye
thamani ya shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta
ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya
Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Vifaa
hivyo vimekabidhiwa leo Ijumaa Mei 8, 2020 na Meneja wa World Vision
Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Zainab Telack katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Massenza
alisema wao kama wadau wa sekta ya afya wanaofanya kazi zao katika
wilaya ya Shinyanga,Kahama na Kishapu jukumu lao kubwa sasa ni
kushirikiana na serikali kupambana na janga la COVID -19 kwa kusaidia
kuimarisha au kuboresha mifumo ya afya.
“Shirika
la World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa tumeleta vifaa vya kujikinga na
COVID – 19 ambavyo vimenunuliwa kutoka MSD lakini Magauni yamenunuliwa
kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kusaidia watumishi wa
sekta ya afya katika mkoa mzima wa Shinyanga”,alisema Massenza.
Alivitaja
vifaa hivyo kuwa Vipaza sauti 243 ‘Megaphones’ kwa ajili ya watoa
huduma ngazi ya jamii kutoa elimu ya Corona vijijini, Barakoa ‘ Surgical
masks’ pea 1000, Vitakasa mikono ‘ Sanitizers’ lita 300, Magauni
maalumu ya kujikinga‘ Personal Protective Equipments – PPE Gouwns’ 60,
Gloves boksi 1000 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 29,013,000/=.
Alisema
mbali na kuchangia vifaa tiba na vifaa kinga, pia wametoa mafunzo kuhusu
ugonjwa wa Corona kwa watoa huduma ngazi ya jamii 117,watoa huduma 132
kwenye vituo vya afya na madiwani 47 wa halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga.
“Kwa
ujumla mchango wetu World Vision Tanzania katika mkoa wa Shinyanga mpaka
sasa umegharimu shilingi 100,083,500/=,na tutaendelea kutoa mchango
mpaka tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili la COVID 19”,alisema.
“Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano inaotupatia katika mapambano dhidi ya COVID -19”,aliongeza Massenza.
Akipokea
vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack alilishukuru
Shirika la World Vision kwa mchango huo wa vifaa tiba akibainisha kuwa
vitawasaidia watoa huduma za afya kuwa na amani wakati wa kwenda
kuhudumia wagonjwa kwa sababu watakuwa na uhakika kuwa na wao
wamejikinga dhidi ya maambukizi ya COVID – 19.
“Mimi
niwashukuru sana World Vision, tuko pamoja na tutaendelea kushirikiana
na naomba muendelee msichoke kutoa mchango kwa sababu ugonjwa huu siyo
wa mtu hakuna anayenyoshewa kidole kuwa huyu atapata. Tunakijikinga
sote, tunajikinga sisi ili pia tusiambukize na wengine lakini na wale
tunaowakinga wakiweza kujikinga na sisi hatuwezi kuambukizwa”,alisema Mhe. Telack.
Mkuu huyo
wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote wanaoendelea
kushirikiana na serikali kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Kwa
upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile
alisema mchango huo wa vifaa utaongeza ari,nguvu na moyo kwa watumishi
wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma stahiki kwa wagonjwa bila
kusita,bila hofu wala mashaka.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Meneja wa World Vision
Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Zainab Telack gauni maalumu la kujikinga na maambukizi
ya COVID -19′ PPE Gouwns’ ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa kwa
ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga
kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia
wagonjwa leo Ijumaa Mei 8,2020 katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa
Shinyanga. Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas
Ndungile. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Zainab Telack akikagua gauni maalumu la kujikinga na maambukizi ya
COVID -19′ PPE Gouwns’ ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na
Shirika la World Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa
sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi
vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Zainab Telack akikagua vazi maalumu la kujikinga na maambukizi ya COVID
-19′ ambalo ni sehemu ya magauni 60 yaliyolewa na Shirika la World
Vision Tanzania kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika
mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid
19’ wanapohudumia wagonjwa.
Kushoto
ni Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack Kipaza sauti na
Gloves.
Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiangalia moja Sanitizer ambayo ni
sehemu ya lita 200 zilizotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa
ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga
kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia
wagonjwa.
Kulia ni
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa John Massenza akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya
shilingi milioni 29 kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya
katika mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona
‘Covid 19’ wanapohudumia wagonjwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza
watumishi wa afya na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu
ugonjwa wa Corona.
Watumishi wa afya katika hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifuatilia zoezi la kukabidhi vifaa tiba na
kinga vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt.
Yudas Ndungile akilishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa mchango
wa vifaa tiba na kinga ambapo alisema mchango huo wa vifaa utaongeza
ari,nguvu na moyo kwa watumishi wa afya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma
stahiki kwa wagonjwa bila kusita,bila hofu wala mashaka.
Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye thamani ya shilingi milioni
29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision Tanzania limetoa kwa ajili
ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga
kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid 19’ wanapohudumia
wagonjwa.
Sehemu ya vifaa tiba na kinga vyenye
thamani ya shilingi milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la World Vision
Tanzania limetoa kwa ajili ya kusaidia watumishi wa sekta ya afya katika
mkoa wa Shinyanga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ‘Covid
19’ wanapohudumia wagonjwa.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment