…………………………………………………………………………..
Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Mbeya, leo wamekabidhi zawadi ya mashine ya cherehani yenye
thamani ya shilingi 1,500,000/= MZRH ikiwa ni mchango wao wa alama ya
upendo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wauguzi duniani.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi(TANNA) tawi la MZRH Bi. Iddah
Sewangi amesema mashine hiyo ya kisasa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na hospitali katika kuboresha huduma na itasaidia kushona
mavazi mbali mbali ya hospitali ikiwemo ushonaji wa mavazi maalum (PPE)
katika mapambano ya janga lilipo sasa la corona.
Akipokea zawadi hiyo kwa niaba ya
uongozi wa hospitali, Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Godlove Mbwanji
amewashukuru wauguzi hao kwa zawadi hiyo ya mashine ambayo na kusema
imekuja kwa wakati wakati sahihi ambapo sasa kuna kazi ya kuendelea
kushona mavazi mbali mbali ya hospitali zikiwemo barakoa.
“.. Kwa niaba ya viongozi ninawapongeza kwa kazi nzuri kubwa na yeye changamoto nyingi ambayo mmekuwa mnaifanya na ninyi kama wawakilishi wa wauguzi wengine walioko kule mawodini, naomba hizi salaam mziifikishe kwao , wauguzi ni jeshi kubwa na tunadhamini sana kazi zenu nzuri kwa ustawi wa hospitali yetu .”
Amesema kuwa katika huduma za matibabu wauguzi ndio wanaokaa na wagonjwa kwa muda mrefu hivyo ni lazima kukutana na changamoto nyingi na kutokana na hilo wameendelea kuonyesha amani upendo na ushirikiano kwa kutimiza majukumu yao ya kufanya kazi pamoja.

Leo dunia inasherehekea kumbukizi
ya kuzaliwa kwa mwasisi wa wauguzi Florence Nightingale, kwa kuwasha taa
ya upendo na kurudia kiapo cha kitaalumakwa kuendelea kuonyesha njia
kwa jamii yenye afya kwa watu wote kizazi cha sasa na kijacho. Pia kutoa
elimu, taarifa na huduma bora kwa jamii yote Kauli mbiu ya maadhimisho
ya siku ya kimataifa ya wauguzi duniani kwa mwaka huu ni Wauguzi, Sauti
inayoongoza Uuguzi kwa dunia yenye Afya.
No comments :
Post a Comment