Muongozaji wa majadiliano Bw. Michael Gwimile
akifafanua jambo wakati wa mkutano wa majadiliano uliowashirikisha wadau
mbalimbali wa Habari ulioandaliwa na MISA-Tan na kufanyika hivi karibuni Jijini
Dodoma
akifafanua jambo wakati wa mkutano wa majadiliano uliowashirikisha wadau
mbalimbali wa Habari ulioandaliwa na MISA-Tan na kufanyika hivi karibuni Jijini
Dodoma
Muongozaji wa majadiliano Mrakibu Msaidizi wa
Polisi Bw. Athumani Mtasha akifafanua
kuhusu nafasi ya polisi katika kudhibiti makosa ya kimtandao na ushirikiano na
vyombo vya Habari wakati wa mkutano wa majadiliano ulioandaliwa na MISA-Tan na
kufanyika jijini Dodoma.
Polisi Bw. Athumani Mtasha akifafanua
kuhusu nafasi ya polisi katika kudhibiti makosa ya kimtandao na ushirikiano na
vyombo vya Habari wakati wa mkutano wa majadiliano ulioandaliwa na MISA-Tan na
kufanyika jijini Dodoma.
Washiriki
wa mkutano wa majadiliano wakiwa wamekaa kwa kuzingatia umbali wa mita moja
wakifatilia majadiliano wakati wa mkutano wa wadau kuhusu changamoto za
matumizi sahihi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
wa mkutano wa majadiliano wakiwa wamekaa kwa kuzingatia umbali wa mita moja
wakifatilia majadiliano wakati wa mkutano wa wadau kuhusu changamoto za
matumizi sahihi ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
**************************************
NA FREDY MGUNDA,DODOMA.
WATANZANIA
wametakiwa kutoa taarifa za uhakika katika mitandao ya kijamii ili
kuondoa upotoshaji ambao umekuwa ukiongezeka kila kukicha na kuzua
taaruki kwa wananchi na
serikali kwa ujumla.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari katika warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini
mwa Afrika kwa hapa nchini Tanzania (MISA -TAN) iliyowakutanisha wadau
mbalimbali wa Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya kuripoti
Habari za COVID-19 bila kuleta taharuki katika Jamii, Msemaji
Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mrakibu Msaidizi Athuman
Mtasha alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa za
mamlaka mbalimbali zisizo wahusu bila uchunguzi matokeo yake husababisha
uchochezi ,takwimu za uongo na kusababisha taharuki katika jamii hivyo
ni vyema watu wakaacha mara moja tabia ya kusambaza taarifa
kwani zinaweza kuwatia hatiani.
Alisema kuwa Kwa
mujibu wa takwimu za mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kumekuwa na
ongezeko kubwa la Matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania na
ongezeko hilo limepanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa
miongoni mwa Wananchi na Taasisi mbalimbali.
Mtasha alisema
kuwa mitandao ya kijamii hususani facebook, twitter, Instagram na
youtube imewawezesha wananchi kuzalisha, kusambaza na kupata taarifa
mbalimbali za matukio yanayojiri katika jamii kwa haraka Zaidi kuliko
redio, televisheni na magazeti.
“Pamoja na fursa
hii kumekuwa na changamoto ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii
zikiwemo upotoshaji, udhalilishaji na matumizi mengine yasiyofaa na Hii
inajidhihirisha kwenye kuongezeka kwa kesi za makosa ya kimtandao katika
miezi ya hivi karibuni” alisema
Afisa sheria
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]Kanda ya kati Joseph Kavishe
amesema mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana na vyombo
vingine likiwemo Jeshi la polisi imeendelea kusimamia kwa ueledi vyombo
vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao .
“TCRA imeendelea
kusimamia kwa ukaribu sana vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine
wa mitandao, kwa Maagizo ya Mhe.Rais kuhusu taarifa za Uzushi yeyote
anayekamatwa lazima taraibu za kisheria kufuatwa,TCRA inasimamia vyombo
vya Habari kwa mashauriano pengine panapokuwa na changamoto Fulani ya
utoaji wa Habari huwa kuna kamati ya maudhui na si kila kosa lazima
kuadhibiwa na makosa mengine kamati ya maudhui hukaa na kuwaonya
wahusika ili kuacha kuleta mkanganyiko katika jamii”amesema.
Mjumbe wa Taasisi
ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Michael John Gumile ambaye pia
ni Mhadhili kutoka chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St.John)
alisema Warsha hiyo ya wanahabari imesaidia wadau wa Habari namna ya
kuandika Habari zitakazosaidia kuondoa taharuki katika jamii hususan
katika kipindi hiki cha Corona.
“Sasa hivi
nchini na Dunia kwa ujumla hivyo wadau wa Habari tumekutana hapa katika
kujenga msingi mzuri ili kuhakikisha taarifa sahihi zinapatikana na watu
kuzifanyia maamuzi na taarifa ambazo haziwezi kuleta mkanganyiko katika
jamii”amesema.
Meneja wa kituo
cha Redio,Dodoma FM ,Zania Miraji ni miongoni mwa wadau wa Habari
waliohudhuria katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya
Habari Kusini Mwa Afrika ,hapa nchini(MISA-TAN) alisema warsha hiyo
imekuwa mwarobaini wa kuwakumbusha waliojifunza kutoka vyuoni na na
maelekezo yaliyotolewa katika warsha hiyo watayafanyia kazi hususan
namna ya kuandika Habari ambazo hazina mkanganyiko pia namna ya
mwanahabari ya kujikinga



No comments :
Post a Comment