
*********************************
Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam imewataka wanafunzi wote wa UDSM watakapofungua chuo
rasmi Jumatatu, Juni Mosi, kuhakikisha wanavaa barakoa (mask) muda wote
wanapokuwa darasani na viunga vya chuo.
Mbali na hilo, wanachuo hao pia wametakiwa kuhakikisha wanapowasili chuoni ni lazima
watumie vitakasa.
“Kila mwanafunzi utakapowasili
chuoni utakutana na vitakasa mikono vya aina mbili vya kukanyaga kwa
miguu na vya automatic ukiweka mikono inatoa sabuni na maji. Kila
mwanafunzi atatakiwa kunawa mikono kila anapotoka sehemu moja kwenda
nyingine,hususani anapoingia darasani na kutoka nje. Kumbuka vitakasa
mikono vitawekwa maeneo yote ya kuingilia na kutoka madarasani na sehemu
zote za mikusanyiko.” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya kwa wanafunzi.
Aidha kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa baada ya kikao kilichoshirikisha uongozi wa serikali ya
wanachuo na Wizara ya Elimu, jana Jumanne, Mei 26 kikao hicho kimeafiki
pia kupunguza muda wa masomo kutoka wiki 15 na saa 45 za awali hadi wiki
12 na saa 36 ili kukamilisha muhula wa pili baada ya muda mwingi
kupotea baada ya janga la Corona kutangazwa.
Taarifa hiyo pia imesema, baadhi
ya shule, taasisi na Ndaki zitapangiwa vipindi kwenye madarasa yaliyopo
katika sehemu zao ili kuondoa uwezekano wa watu kukusanyika.
Mitihani ya kumaliza muhula
inatarajiwa kuanza rasmi Agosti hadi Agosti 28 huku wanafunzi wote
wakitakiwa kuipakua ratiba hiyo ya masomo kaunzia leo, Jumatano kupitia
tovuti ya chuo.
Kwa upande wa vyuo vya ualimu,
taarifa hiyo imesema kutakuwa na mabadiliko ya mafunzo ya vitendo ambayo
itaanza rasmi Agosti 31 na kuhitimisha Oktoba 9 ambapo itakuwa ni
pungufu ya wiki mbili na awali.
Kwa upande wa wanafunzi wa
Kimataifa wanakaribishwa kuendelea na masomo lakini kwa wale ambao nchi
zao hazitawaruhusu kutokana na ‘Lockdown’ watatakiwa kuandika barua ya
kuahirisha muhula na kuja kusoma mwaka unaofuata wa masomo 2020/2021.
No comments :
Post a Comment