Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba kulia akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella leo vyenye thamani ya sh.milioni 70 walivyovitoa kwa kushirikiana
na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira ya Bahari (Marine Parks and Reserves
Tanzania) kushoto ni Mhifadhi Ufundi,Ununuzi na Ufuatiliaji wa Hifadhi za
Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Clever Charles Mwaikambo

MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kupokea
vifaa hivyo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba
Ndomba
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba akizungumza kabla ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella

Ndomba katikati akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella

MKUU wa Mkoa wa Tanga akisanitizer kabla ya kufanya makabidhiano hayo ambaye
anamueweka kwenye mkono ni Afisa Habari wa TASAC Nicholous Kinyariri

SEHEMU ya vifaa hivyo
*********************************
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella leo
amekabidhiwa vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari vyenye thamani ya
shilingi milioni 70 vilivyotolewa na Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania(TASAC) pamoja na Shirika la Uhifadhi Mazingira ya Bahari(Marine
Parks and Reserves Tanzania).
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC,Emmanuel Ndomba amesema kuwa vifaa hivyo ni vya
aina mbili na ni vya huduma ya kwanza vya kudhibiti uchafuzi wa
mazingira ya bahari unaosababishwa na kumwagika kwa mafuta.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni kifaa cha
kuwezesha vifaa vingine kinachoitwa ‘power parks’ ambacho kinaendesha
vifaa vya kutenganisha maji na mafuta kinachoitwa ‘skeamer’ na kifaa cha
kusukumia maji.
Amesema kuwa TASAC na Shirika la Uhifadhi
Mazingira ya Bahari kwa pamoja wametoa vifaa hivyo kwa malengo makuu
matatu ambayo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na
uchafuzi wa mazingira ya bahari,kujenga uchumi wa nchi kwa watu
wanaoishi katika mazingira ya bahari na kusaidia mafunzo ya usafi wa
mafuta yanayomwagika baharini kwa wadau wa mazingira ya bahari.
” Sisi TASAC kwa kushirikiana na wenzetu wa
Marine Parks tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali katika kutunza
mazingira ya bahari,”alisema.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine
Shigela amewashukuru TASAC na Marine Parks kwa msaada huo na kusema kuwa
umekuja wakati muafaka haswa katika bandari ya Tanga haswa katika
kipindi hiki ambacho bandari hiyo ipo kwenye upanuzi na pamoja ujio wa
bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda.
Amesema kuwa vifaa hivyo ni matokeo ya ahadi
iliyotololewa mwezi Septemba mwaka jana wakati wa mafunzo ya usafi wa
mazingira ya bahari yaliyotolewa na TASAC .
Amesema kuwa vifaa hivyo vitapatikana kwa muda
wa saa 24 ndani ya siku saba za wiki pindi mafuta yatakapomwagika iwe
rahisi kuyaondoa kwa wakati.
Aidha,amewataka watumishi na wadau wa wote wa
bahari kutimiza wajibu wao na kutaka ikiwezekana kutenga bajeti kwa
ajili ya ununuzi wa vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari.
Kuhusu upanuzi wa bandari ya Tanga, Shigella
alisema kuwa tayari mashine ya kuchimba kina cha bahari umemaliza kazi
yake kinachofuata ni kuletwa kwa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa gati
No comments :
Post a Comment