Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Manispaa ya Singida, Alhaji Sheikh Hamisi Kisuke.
Na Dotto Mwaibale, Singida
Hayo
yalisemwa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Manispaa
ya Singida, Alhaji Sheikh Hamisi Kisuke, wakati akizungumza na waandishi
wa habari katika sherehe ya Idd Pili.
Kisuke alisema kushirikiana, kupendana na kuheshimiana baina ya Waislamu na Wakristo ndio kunadumisha hali hiyo hapa nchini.
Alisema
Waislamu na Wakristo wamekuwa wakijumuika pamoja katika sherehe zao
mbalimbali kama za Idd na Krismas na kila upande ukiona shehere hizo
kama ni zake.
” Wakati wa sherehe hizo Waislamu wamekuwa wakiwaalika wakristo na wakristo nao wamekuwa wakiwaalika waislamu” alisema Kisuke.
Kisuke
alisema jambo hilo liliasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius
Nyerere ambaye alisema Serikali ya Tanzania haina dini ila wananchi wake
ndio wanadini.
Akizungumzia
kuhusu ugonjwa wa Corona Kisuke alimpongeza Rais John Magufuli, Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na viongozi
wengine kwa hatua walizozichukua za kukabiliana na ugonjwa huo.
Alisema
wao katika ibada ya Idd walifuata maelekezo yote ya kuchukua tahadhari
yaliyotolewa na Mufti Mkuu wa Tanzania, Aboubakary Bin Zubeir, ambapo
kila Muislamu aliswali katika msikiti wake badala ya kukusanyika katika
viwanja maalumu kama ilivyozoeleka.
“Wakati
wa ibada ya Idd tulichukua tahadhari zote kama kunawa mikono kwa maji
tiririka, kuvaa barakoa na kuswali kwa kuzingatia umbali wa mita moja
huku wakiwepo maafisa afya ambao walikuwa wakisimamia zoezi hilo la
kuchukua tahadhari” alisema Kisuke ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Misuna.
No comments :
Post a Comment