Rais
Trump amekatisha mkutano na waandishi baada ya kukerwa na swali la
Mwandishi wa CBS Weijia Jiang aliyemuhoji ni kwanini amekuwa anashindana
kwa kujigamba kuwa USA inaongoza kupima corona kuliko wote wakati wana
vifo zaidi ya Elfu 81.
Trump alimjibu hapaswi kuulizwa kwanini Wamarekani wengi wanazidi
kupoteza maisha wakati sehemu nyingi duniani watu wanapoteza maisha
hivyo sio swala la ajabu huku akisisitiza kuwa swali hilo wanapaswa
kuulizwa China kwa kuwa wao ndio wameleta Corona na sio Yeye.
Baada ya kuona mwandishi anahitaji kujibiwa swali lake Trump akaona isiwe tabu akaamua kuondoka zake.
Trump aliulizwa kuwa “Why is this a global competition to you if every
day Americans are still losing their lives and we’re still seeing more
cases?”
No comments :
Post a Comment