Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa
Yunus Mgaya alisema kuwa Wanapendekeza aina tatu za mchanganyiko wa
mimea tiba kutengeneza joto tiba au mvuke kwaajili ya kujifukiza
kuondokana na virusi vya magonjwa mbalimbali ikiwemo hili la virusi vya
Corona.
Aliutaja aina ya kwanza ya
mchanganyiko wa mimea ambayo wananchi wanaweza kuutumia ni mchanganyiko
wa majani ya mkaratusi, majani ya kivumbasi au kashwagala na majani ya
mchaichai.
Aina ya pili ni mchanganyiko wa
majani ya mchaichai, karafuu, tangawizi iliopondwapondwa na majani ya
mlimao. Aliutaja aina ya tatu ni kuwa ni mchanganyiko wa majani ya
mwarobaini, majani ya mpera, mchaichai na majani ya mlimao.
Kwa mujibu wake, tiba joto hiyo au
mvuke ni muhimu kwani inasaidia kuongeza kinga ya
mwili, kufungua njia
ya hewa na kukirarua kirusi cha corona kama bado kiko kwenye njia ya
hewa na hakijaingia kwenye mapafu.
Alisema tiba ya kujifukiza
haisaidii kama tayari kirusi cha corona kimeshaingia kwenye mapafu,
hivyo mgonjwa anatakiwa kupewa matibabu mengine ikiwemo antibiotic.
Prof.Mgaya alishauri mvuke huo
unahitaji Joto la nyuzi 50-70. Anasema “Joto la mvuke linatakiwa liwe
kati ya nyuzi 50 hadi 70, likizidi linaweza kuumiza njia ya hewa, mtu
anatakiwa avute mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni, watu wazima
wavute kwa dakika nane hadi kumi na watoto kuanzia umri wa miaka saba
wavute kwa dakika mbili hadi nne, watoto chini ya miaka saba
hawaruhusiwi kutumia tiba hii,” alisema Profesa Mgaya.
Kwa kuwa mvuke una kiasi kidogo
cha hewa ya oksijeni, alisema watu wenye matatizo ya kupumua hawapaswi
kutumia tiba hiyo kwani wanaweza kupoteza maisha, pia wanaotumia
wasijifukize wakati sufuria iko kwenye jiko la mkaa bali iwekwe chini au
mahali pengine kwa kuwa mkaa hutoa hewa yenye sumu hatari kwa binadamu.
Kuhusu maandalizi ya dawa hiyo,
Profesa Mgaya alisema hatua ya kwanza ni kuchemsha maji ya lita tano au
kumi hadi yachemke, kisha yawekwe majani na kuyafunika na kuyachemsha
kwa dakika tano tu.
Alisema dawa ikichemshwa kwa zaidi
ya dakika tano inakuwa imepikwa na haifai kwa tiba kwa sababu
virutubisho muhimu vinakuwa vimepotea kwa njia ya mvuke.
Alisema wakati wa kujifukiza mtu
anaweza kujifunika kwa blanketi au shuka au taulo zito ili mvuke
usipotee, na baada ya kujifukiza muhusika asipewe maji baridi ya kunywa
kwani ataharibu tiba bali apewe glasi ya maji ya moto au chai.
Kuhusu kipimo cha dawa hizo,
alitoa kipimo kwa mchanganyiko wa kwanza tu ambapo mtu anatakiwa atumie
gramu 50 za majani ya mkaratusi na gramu 50 za kivumbasi na gramu 20 za
mchaichai.
No comments :
Post a Comment