……………………………………………………………………………………………..
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
wamekabidhi jengo la makazi ya watumishi kwa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) lililopo katika Makao Makuu ya Shamba la Miti Sao Hill –
Mafinga.
Jengo hili limejengwa kwaajili ya
makazi ya watumishi wa TFS – Shamba la Miti Sao Hill ambalo litatumika
kwa makazi ya familia mbili za watumishi (semi detarch). Akizungumza
wakati wa kukabidhi jengo hilo Meneja wa NHC Mkoa wa Iringa Bw. Repson
Yosiah amesema kuwa wamekamilisha jengo hili kwa wakati ili litumike kwa
matumizi yaliyokusudiwa.
Naye Mwakilishi kutoka TFS
Mhandisi Kaston H. Sanga amewashukuru NHC kwa kukamilisha jingo hili kwa
wakati na hivyo linaenda kusaidia watumishi waliopo katika Shamba la
Miti Sao Hill ikiwa ni sehemu ya mikakati ya TFS.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill
Bw Juma Mwita Mseti amesema kuwa anaishukuru TFS kwa kuendelea kuona
umuhimu wa kujenga makazi ya watumishi kwani inasaidia kuboresha
utendaji wa kazi ikiwa watumishi wote kukaa karibu na eneo
wanalolifanyia kazi.
Jengo hili limejengwa na TFS
kupitia NHC kwa gharama ya Tsh 229,369,589 ikiwa ni sehemu ya mikakati
ya taasisi ili kuboresha miundo mbinu ambayo husaidia katika utendaji wa
kazi wa kila siku ili kuongeza ufanisi na hivyo kufikia malengo ya
taasisi.
#misitukwanza
#misitukwanza
No comments :
Post a Comment