…………………………………………………..
Na Magreth Mbinga,Dar es Salaam
Kuanzia kesho tunakamata wafanyabiashara wote wanaouza sukari kwa bei ya juu tofauti na iliyotolewa na Serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda wakati
akifanya ziara katika
wilaya ya Kigamboni kukagua uboreshaji wa awamu ya pili ya daftari la
kudumu la mpiga kura.
Makonda amesema hakuna sababu ya
kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kupandisha bei ya sukari ambapo bei
elekezi ya Serikali ni shilingi 2600 kwa kilo moja lakini watu wanauza
hadi sh 3500 kwa kilo.
Aidha amewataka wananchi
wasitumie hotuba ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John
Magufuli kusambaza taarifa mbaya na zakupotosha jamii ya Tanzania.
“Lengo la Mh Rais kupima sampuri
za wanyama na matunda ni kukagua kipimo ambacho kinatumika kupima
ugonjwa wa Corona na sio wanyama na mimea imeathirika na ugonjwa huo
kuleni matunda kwani yanajenga afya ya mwili” amesema Makonda.
Hata hivyo Makonda amemshukuru
Rais Magufuli kwa kuwapatia heshima wananchi wa Dar es salaam kwa
kuwapatia ruhusa waendelee kufanya kazi kwasababu wananchi wengi
wanategemea watoke ili wapate pesa ya kula kwa siku.
“Tusimuangushe Rais Magufuli najua
wapo baadhi ya watu waliotaka mji ufungwe ili tusimuangushe Rais watu
tufate maelekezo ya wizara ya afya ili kulinda heshima ya kauli yake”
amesema Makonda.
No comments :
Post a Comment