Kamishna Jenerali wa Magereza,
Suleiman Mzee(kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) leo
Mei 8, 2020 alipofika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma
kabla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika Gereza
Kuu Isanga Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Suleiman Mzee(kushoto meza kuu) akizungumza jambo na Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony
Mavunde (kulia) leo Mei 8, 2020 alipofika Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza jijini Dodoma kabla ya kukabidhi vifaa vya kujikinga na janga
la corona katika Gereza Kuu Isanga.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
nje ya Gereza akikabidhi vifaa vya kujikinga na janga la corona katika
Gereza Kuu Isanga, jijini Dodoma. Mhe. Mavunde amekabidhi msaada
uliojumuisha vifaa mbalimbali ikiwemo sabuni, ndoo za maji pamoja na
vitakasa mikono(Sanitizer).
Baadhi ya vifaa hivyo
vilivyokabidhiwa katika Gereza Kuu Isanga na Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma,
ACP. Keneth Mwambije akimshukru Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde(kushoto) baada
ya kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na janga la corona
Kamishna Jenerali wa Magereza,
Suleiman Mzee(kushoto) akiagana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde mara baada ya
mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini
Dodoma (Picha zote na Jeshi la Magereza).
……………………………………………………………………
Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma.
GEREZA Kuu Isanga, Dodoma leo
limepokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na
Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony
Mavunde (Mb) kwa ajili ya kusaidia kupambana na janga la Corona
magerezani.
Akizungumza jijini Dodoma mara
baada ya kupokelewa kwa msaada huo uliojumuisha sabuni, ndoo za maji
pamoja na vitakasa mikono(Sanitizer), Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Suleiman Mzee amemshukuru Naibu Waziri Mavunde pamoja na Wadau
mbalimbali wa Jeshi hilo wenye nia njema ambao wanaendelea kujitokeza
kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukabiliana na janga la corona
nchini.
“Mhe. Mavunde nikushukuru sana kwa
msaada wa vifaa hivyo ulivyovikabidhi leo katika Gereza Kuu la Isanga,
Dodoma kwani vitasaidia maafisa, askari pamoja na wafungwa na mahabusu
katika kujikinga na corona magerezani”, alisema Kamishna Jenerali
Suleiman Mzee.
Akikabidhi msaada huo wa vifaa,
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira
Mhe. Anthony Mavunde (Mb) alimuahidi Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini kwamba huo ni mwanzo na yuko tayari wakati wowote kutoa mchango
wake pale itakapohitajika kufanya hivyo.
Wakati huo huo, Gereza hilo mapema
leo limepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kibinadamu kwa ajili ya
wafungwa na mahabusu vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5,500,000/=
ambavyo vimetolewa kwa pamoja na MTANDAO wa Watumishi wa Umma Wanawake ujulikanao kama Viongozi Wanawake Wanaoibukia Tanzania(Emerging Women Leaders in Tanzania – EWLT).
Kufuatia kuripotiwa uwepo wa ugonjwa wa corona(COVID -19)
nchini, Jeshi la Magereza Tanzania Bara limeendelea kuchukua hatua za
tahadhari ikiwemo kusitisha kwa huduma zote za kutembelea wafungwa na
mahabusu pamoja na kuletewa chakula mahabusu waliopo magerezani. Aidha,
Jeshi hilo linaendelea kuchukua tahadhari na hatua kwa kadri
litakavyoona inafaa sambamba na kuzingatia miongozo mbalimbali
inayotolewa na Serikali dhidi ya janga hilo.
No comments :
Post a Comment