Kutokana
na virusi vya corona vinavyoendelea kuisumbua dunia, Wizara ya Utalii
na Maliasili imesema mapato katika sekta hiyo yameshuka kutoka Sh
trilioni 2.6 zilizotarajiwa kukusanywa
Pia
taasisi zilizokadiriwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 132.1 zinatarajia
kukusanya Sh bilioni 33.5 ikiwa ni anguko la asilimia 75.
Vilevile,
Serikali imesema kama hali haitatulia hadi Oktoba, ajira za moja kwa
moja katika sekta ya utalii zitashuka kutoka 623,000 hadi kufikia
146,000 na watalii watashuka kutoka 1,867,000 waliotarajiwa hadi
437,000.
Kauli
hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na
matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/21.
Dk. Kigwangalla alisema sekta ya utalii imeathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na corona.
Alisema
wizara ilifanya tathmini ya awali (rapid assessment) iliyojikita katika
kipindi cha tangu ugonjwa huo uanze hadi Aprili 6, mwaka huu.
Dk.
Kigwangalla alisema tathmini hiyo ilibaini kuwa madhara makubwa ya
corona katika sekta ya utalii yalianza kuonekana mwanzoni mwa Machi,
tofauti na Februari na Januari, mwaka huu ambapo hali ilikuwa shwari.
Alisema tathmini ilibaini mashirika 13 ya ndege yalisitisha safari za
kuja nchini tangu Machi 25, mwaka huu hivyo kuondoa uwezekano wa
kuendelea kupata watalii kutoka nje ya nchi.
Dk.
Kigwangalla alisema mashirika yaliyositisha safari zake ni pamoja ni
Emirates, Swiss, Oman Air, Turkish, Egyptian Air, South African Airways,
Rwandair, Qatar, Kenya Airways, Uganda Airlines, Fly Dubai na KLM
Alisema
NCAA ilikadiria kukusanya Sh bilioni 162.7, kwa sasa itakusanya Sh
bilioni 58, TFS ilikadiria Sh bilioni 153.6, sasa ni Sh bilioni 121 na
Tawa ilikadiria Sh bilioni 58.1 sasa ni Sh bilioni 22.
No comments :
Post a Comment