Idadi
ya visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona visiwani Zanzibar
imeongezeka na kufikia 9, baada ya hii leo kutangazwa visa vipya viwili,
ambapo wote ni wa Tanzania na hawana historia ya kusafiri nje ya nchi
siku za hivi karibu na kwamba wote kwa pamoja walianza na homa, mafua na
kifua.
Taarifa
hiyo imetolewa leo Aprili 10, 2020, na Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad
Rashid Mohamed, na kusema kuwa mgonjwa wa kwanza ana umri wa miaka 33
na ni mkazi wa Mwanakwerekwe, ambapo aliripotiwa akiwa na homa kali,
mafua na kifua.
"Mgonjwa wa pili ana miaka 24, mkazi wa Mtendeni na wagonjwa hawa wote
hawana historia ya kusafiri nje ya nchi hivi karibuni, aidha Wizara
inaendelea kuwafuatilia wengine 86 waliowahi kukutana na hawa wagonjwa,
pia kuna watu 252 waliorudi kutoka nje ya Tanzania wamewekwa Karantini
Unguja na Pemba" amesema Waziri wa Afya Zanzibar
No comments :
Post a Comment