Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) na Waziri wa Viwanda na Bishara
Mhe Innocent Nashungwa (Kulia) wakifuatilia hoja za washiriki wa kikao
kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020. (Picha Zote Na Eliud Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara)
Sehemu
ya wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara
pamoja na AGRA wakifuatilia hoja za washiriki wa kikao kazi cha kujadili
namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Nashungwa (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
Mshauri wa masuala ya Maendeleo ya Viwanda vya Kilimo wa Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) Ndg Peniel Lyimo akichangia
mada wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa cha
kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
******************************
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wataalamu
kutoka Wizara ya Kilimo kadhalika, Wizara ya Viwanda na Bishara, na
Taasisi za soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (TanTrade) na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika
(AGRA) wamekutana Jijini Dodoma kujadili kwa pamoja namna ambavyo Wizara
hizo mbili zinaweza kuongeza mshikamano na weledi wa kiutendaji kwa
ajili ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda.
Katika
kikao hicho kilichotuama katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu kama
Kilimo IV kikiongoza na mawaziri kutoka pande mbili, Waziri wa Kilimo
Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent
Nashungwa (Mb) kwa pamoja wamesisitiza ulazima wa wataalamu hao
kuunganisha nguvu kwa pamoja baina ya Wizara na Taasisi za umma na
binafsi ili kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Uzalishaji,
uhifadhi, Ubora kwa Mazao ya kimkakati na mchanganyiko.
Akizungumza
katika kikao hicho Waziri wa Kilimo Mhe Japhet hasunga (Mb) amewataka
Wataalamu hao kuimarisha intelijensia ya masoko kwa kutumia mbinu
mbalimbali ikiwemo na ufuatiliaji wa karibu wa mwenendo wa masoko ya
Mazao na bidhaa ulimwenguni.
Hasunga
amesema kuwa pamoja na mikakati ya masoko lakini wataalamu hao
wanaweza kujadili na kuona namna ya kuimarisha uhifadhi wa Mazao ya
wakulima baada ya kuvuna kwani Barani Afrika nafaka myingi hupotea mara
baada ya kuvuna.
Amewataka
wataalamu hao pamoja na mambo mengine amewataka kuhakikisha kuwa
wanaimarisha miundombinu ya masoko ikiwemo maghala ya kisasa ya
kuhifadhia Mazao na bidhaa.
Naye,
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa
intelijensia ya masoko inapaswa kuhakikisha kwa haraka inatumia Balozi
za Tanzania nje ya nchi katika kutafuta fursa za masoko ya Mazao na
bidhaa pamoja na kuanzisha madawati ya biashara (Trade/Commercial
attache) Kwenye balozi hizo.
Pia
amesema mpango mkakati wa kuwaunganisha wakulima na wasindikaji ndani
na nje ya nchi ni muhimu kutekeleza haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja
na kujenga uwezo zaidi katika kuongeza Uzalishaji wenye tija ili kukidhi
nahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
Kadhalika
Waziri Bashungwa ameongeza kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) wanapaswa kukutana
na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kujadili uimarishaji wa masoko ya
Mazao mbalimbali.
Pamoja
na mambo mengine Waziri Bashungwa ameitaka Taasisi ya kuendeleza Kilimo
Barani Afrika (AGRA) kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya Kilimo
ili kutafuta ufunguzi wa namna ya kuimarisha masoko ya Mazao ya wakulima
nchini.
No comments :
Post a Comment