Friday, April 10, 2020

WATU WATANO MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWALIMU MKOANI DODOMA



…………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kamanda wa Polisi JESHI La Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema watu watano wanashikiriwa na jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chilungulu, Wilaya ya Bahi, Eradius Mgaya(41) na kumtupa kwenye shamba la shule.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari Jijini Dodoma, ,amesema tukio hilo
lilitokea Aprili 7, mwaka huu katika kijiji cha Chilungulu.
Muruto amesema kuwa Mwalimu huyo alipigwa na kitu chenye ncha kali na kutupwa kwenye shamba la shule hiyo.
“Hawa watuhumiwa walimvizia njiani alipokuwa akirejea nyumbani kwake, jeshi la polisi bado tunachunguza chanzo cha kifo na watuhumiwa tunawashikilia hadi hapo tutakapokamilisha uchunguzi,”ameleza Muruto.
Katika hatua nyingine, Mkazi wa Image jiji la Dodoma Godfrey Shirima (22) anashikiliwa kwa kukutwa na silaha aina ya Bastola yenye namba za usajili 016975 ambayo anamiliki kinyume na sheria huku akiitumia katika uhalifu.
Hata hivyo,Muruto amesema kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika
Muroto hakutaja majina ya watuhumiwa hao na kudai kwamba bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
Wakati huo huo, Kamanda huyo ameonya mikusanyiko isiyo ya lazima itakayosababisha msongamano hasa wakati huu ambapo kila raia anapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
“Nitoe rai kwa Wazazi kuwalinde watoto wao na wasiwaruhusu kwenda kwenye mikusanyiko kama ilivyozoeleka, pia watu wajiepushe na ulevi wa kupindukia na kuchukua tahadhari ya usalama barabarani,”Muroto ametoa wito.

No comments :

Post a Comment