Mkuu
wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo akizungumza na viongozi mbalimbali
wa vijiji na vitongoji (hawapo pichani) vinavyopaka na mwambao wa ziwa
Tanganyika katika kata za Korongwe na Kabwe Wilayani Nkasi
Afisa
Afya wa Mkoa wa Rukwa Kennedy Kyauke akitoa elimu ya hatua za kunawa
mikono kwa viongozi mbalimbali wa vitongoji, vijiji na kata (hawapo
pichani) wakati wa Kikao kifupi baina ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa na
viongozi hao.
Viongozi
mbalimbali wa vijiji na vitongoji vinavyopaka na mwambao wa ziwa
Tanganyika katika kata za Korongwe na Kabwe Wilayani Nkasi, wakisikiliza
kwa makini elimu na maelekezo wanayopewa ili kuilinda mipaka ya nchi na
kujilinda dhidi ya ugonjwa wa Corona. Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka viongozi wa vitongoji,
vijiji pamoja na watendaji wao wa kata za Korongwe na Kabwe kuhakikisha
wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao kuwa mstari wa mbele katika
kuilinda nchi kutokana na ugonjwa wa Corona kwa kuzuia uingiaji holela
wa wageni wanaoweza kuuleta ugonjwa huo kutoka nchi za jirani.
Mh
Wangabo amesema kuwa hadi sasa mkoa wa Rukwa umewaweka Karantini watu
49 ambapo kati ya hao watanzania 36 na wageni 13 ambao walipita katika
bandari na mipaka rasmi ya mkoa huo na kusisitiza kuwa katika
utekelezaji wa kuwaweka watu Karantini hauangalii uraia wa mtu wala
hadhi yake, na kuongeza kuwa inachokijali serikali ni usalama wa
wananchi wake dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona.
“Waende
wakapite katika maeneo ambayo ni rasmi, waje hapa kwenye bandari ya
Kabwe, wapite hapo na taratibu nyingine za kiafya zitafanyika, lakini
sio kwenye bandari bubu huku, bandari bubu ni marufuku kutumika, ndani
ya wilaya hii ya Nkasi kuna bandari bubu 46, Nkasi peke yake na katika
kata zenu mbili hizi, ya Korongwe na Kabwe kuna bandari bubu 13, ndio
maana nikasema viongozi ninyi wa kata mbili hizi mje hapa, ili muone
umuhimu wa kuzuia watu kiholela holeal kuja kwenye bandari hizi bubu,”
Alisisitiza.
Mh.
Wangabo ameyasema hayo wakati wa kikao na wenyeviti wa vitongoji na
vijiji vyenye bandari bubu pamoja na watendaji wa kata Kabwe na Korongwe
zinazobeba vijiji hivyo katika kikao kilicholenga kutoa elimu ya
ugonjwa wa Corona kwa viongozi hao pamoja na kutoa maelekezo ya serikali
dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo.
Kwa
upande wake Kamanda wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Kamishna
Msaidizi Elizeus Mushongi alitahadharisha matumizi mabaya ya madaraka ya
viongozi hao ambao huwapokea wageni hao na kuwaruhusu kuingia katika
nchi bila ya kufuata utaratibu wa serikali na kuongeza kuwa matumizi ya
bandari bubu ni haram una hivyo atakayekamatwa anahalalisha matumizi ya
bandari hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
“Wageni
kutoka nje ya nchi, iwe Kongo, iwe Burundi, iwe Zambia, mnawapokea kule
na nyinyi ndio mnakuwa maafisa uhamiaji, mnakuwa maafisa forodha, kila
kitu mnamaliza wenyewe kule, sasa kama mtampokea mtu anaumwa ule
ugonjwa, ninyi ndio mtakaoanza kuupokea ule ugonjwa kabla ya wote na
bila ya kujua mtaenda kuambukiza familia na familia kama dokta
alivyosema, niwaombe sana msipokee watu kutoka nje ya nchi kama
hawajapita katika vituo vilivyoainishwa kisheria,” Alisema.
Aidha
wakati akitoa salamu zake kwa mkuu wa mkoa, Diwani wa Viti Maalum Mh.
Christina Simbakavu alisema kuwa kuna baadhi ya watu wenye ndugu zao
nchi ya jirani ya Kongo huwa na kawaida ya kuingia katika vijiji hivyo
nyakati za usiku na ndugu zao huwapokea katika utaratibu ambao unaweza
kuhatarisha maisha yao.
“Kuna
boti zinazoingia usiku kama alivyotamka mjumbe wa Kijiji cha Kalila,
zile boti zinaingia lakini wenyeji wenye ndugu zao kutoka nchi jirani ya
kongo wanawapokea katika mazingira ambayo sio Rafiki sana na hawatoi
taarifa, na hili nalo linafukuta lakini hatujapata uhakika uliowazi,
tunajaribu kuongea na wananchi kuwa tusipokee wageni wa aina yoyote na
nawaomba viongozi wangu tuhamasishe utumiaji wa maji na sabuni kunawa na
katika nyumba zetu tuweke vifaa hivyo,” alisema.
Naye
Diwani wa Kata ya Korongwe Mh. Venus Bamilitwaye wakati akitoa neno la
shukurani ka mkuu wa mkoa wa rukwa aliwasisitiza viongozi wa kata hizo
kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kulinda bandari bubu
pamoja na kuzuia uingiaji wa kiholela wa wageni jambo ambalo ni hatari
kwa afya ya wananchi wa mkoa wa Rukwa na Tanzania.
No comments :
Post a Comment