Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa matunda na nyanya kando ya mnada wa mifugo
wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo
kujionea namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu
kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora
ya kunawa wa Mikono kabla ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu
kitachotumika kuhudumia wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa
huo Wilayani Kishapu jana alipofika katika kituo hicho kujionea namna bora ya uzingatiaji w
Na Anthony Ishengoma- Sinyanga
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack amewataka wazazi na walezi
mkoani Shinyanga kutowaruhusu watoto wadogo kwenda katika mikusanyiko
hususani minada ya mazao na mifugo kama hatua muhimu ya kuwakinga na
maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Mkuu
wa Mkoa ameyasema hayo wakati alipotembelea mnada wa mifugo wa Muhunze
ulioko katika Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa
lengo la kujionea utekelezaji wa agizo la serikali linalowataka wananchi
kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa corona ikiwemo kuweka
maji na sabuni katika maeneo yanayokutanisha watu wengi pamoja na
kukaa umbali wa mita moja.
Bi.
Tellack ameonya kuwa huu si wakati wazazi kutembea na watoto wao
kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kuwataka kusubiri
mpaka wakati ugonjwa huu utakapokuwa umedhibitiwa kwani uwezo wa watoto
kujikinga ni mdogo sana.
Pamoja
na agizo hilo la Mkuu wa Mkoa kwa wakazi na wafanyabiashara katika
minada ya mifugo pia hakuridhishwa na hatua za zuinazochukuliwa na
uongozi wa mnada huo za kuhakikisha wale wote wanaoingia mnadani hapo
wanasafisha mikono yao baada ya kujionea mnada huo ukiwa na njia zaidi
ya moja ya kuingia mnadani hapo na kutoa nafasi kwa baadhi ya watu
kujipenyeza ndani ya eneo hilo bila kuchukua tahadhari ya kujikinga na
Corona.
Bi.
Tellack amewataka wafanyabiashara mnadani hapo kuhakikisha wanajikinga
na maambukizi hayo kwa kila mmoja kunawa mikono yake kila mara na
kuhakikisha wanakuwa na vitakasa mikono (sanitizers) kwa vile wanao
uwezo wa kuvinunua kama hatua muhimu ya kujikinga na hatari ya
maambukizi hayo.
‘’Nunueni
vitakasa mikono kwa ajili ya usalama wenu kwa sababu hamuwezi kukosa
fedha ya kununua ya kiasi cha shilingo elfu nne na miatano na hata kama
ni shilingi elfu kumi kwa ajili ya kujikinga na kuwakinga
wengine.’’Aliendelea kusema kiongozi huyo wa Mkoa.
Agizo
kama hili pia lilitolewa na Mkuu wa Mkoa kwa wafanyabiashara ndogo
wanaofika eneo la mnada kwa lengo la kujipatia kipato tofauti na mifugo
inayouzwa mnadani kuhakikisha wanakuwa na maji na sabuni vinginevyo
watozwe faini kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo muhimu la Serikali.
Pamoja
na kutembelea mnada huo Bi. Tellack pia alitembelea Kituo cha Afya cha
Wilaya ya Kishapu kilichoandaliwa kama sehemu maalumu ya kupeleka
wagonjwa wa corona endapo watabainika Wilayani humo kama hatua muhimu ya
kujionea ni namnagani Wilaya ya Kishapu imejipanga kukabiliana na
ugonjwa huo.
Akiwa
katika kituo hicho cha Afya Mkuu wa Mkoa amejionea vifaa
vnitakovyotumiwa na waudumu wa Afya kujikinga na kuwahudumia wagonjwa na
kuwataka wahudumu hao kuwa tayari kwa lengo la kukabiliana na kuhudumia
wagonjwa hao kwa tahadhari kubwa.
Mnada
huo unaowakutanisha wafanyabiashara wa mifugo kutoka sehemu mbalimbali
za mkoa wa Shinyanga na mikoa jilani ufanyika kila Siku ya Alhamisi na
kuvuta wafanyabiashara wa aina nyingine nje na ndani ya mnada huo ambao
pia wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuweka vitakasa mikono katika
maeneo yao ya biashara
No comments :
Post a Comment