………………………………………………………….
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Imeelezwa kuwa
Waandishi wa habari nchini wapo kwenye kipindi kigumu cha kutekeleza
majukumu yao wakati huu wa mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19 kiuchumi na
wadau wametakiwa kujitokeza kusaidia kada hiyo ili iweze kutoa taarifa
sahihi na kweli.
Kwa mujibu wa Mdau wa
maendeleo jijini Arusha Mwanasheria Maarufu Albert Msando na mmiliki wa
The Don ambaye ametoa Barakoa na vitakasa mikono kwa klabu ya waandishi
wa habari Mkoa wa Arusha (APC) ikiwa ni kusaidia mapambano dhidi ya
Ugonjwa wa Covid 19.
Msando akizungumza
mara baada ya kutoa msaada huo amesema kuwa kada ya uandishi wa habari
ni muhimu Sana kutoa Taarifa za Ugonjwa wa Covid 19 lakini wao wamekuwa
wakishindwa kutoa taarifa kutokana na changamoto zao kipindi hichi cha
janga la Corona
Aidha alisema kuwa
imekuwa shida Sana kupata taarifa sahihi za Ugonjwa huu huku hali ikiwa
inazidi kuwa mbaya na kipindi hichi jamii inahitaji taarifa zaidi ili
kuiondoa kwenye taharuki ni muhimu kwao wanahabari kuwezeshwa hata nauli
ya kutoka eneo moja kwenda jingine itaisaidia jamii kupata taarifa
sahihi sio Bora taarifa.
Alisema kuwa ni
muhimu kwa waandishi kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo husika na
kuzitoa utaona ni Jambo dogo Ila kila moja amekuwa na taharuki kutaka
kujua taarifa kupitia kwenu nanyi ni watu muhimu Sana ikitoka wataalamu
wa Afya ni nyinyi.
“Wadau wajitokeze
kusaidia kwani waandishi wa habari wapo katika wakati mgumu Sana
Kiuchumi katika kipindi hiki Cha Ugonjwa wa Covid 19 na jamii inahitaji
taarifa za hali ya Ugonjwa huo huku waandishi wakiwa taabani kiuchumi
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku”alisisitiza
Aliwataka waandishi
wa habari kusema ukweli kuhusu idadi ya watu wanaokufa waliopata Ugonjwa
wa Covid 19 kwani jamii inapata taarifa sahihi kutoka kwao hivyo
Amewataka kutumia uwezo wao wote na kufanya kazi hiyo kwa weledi.
Aliwakumbusha wadau
wa maendeleo kuendelea kusaidia waandishi wa habari ili waweze kuwapatia
wananchi taarifa za kina na sahihi kuhusiana na janga hili ili kuondoa
taaruki miongoni mwa jamii.
Naye Mwenyekiti wa
chama cha wa ndishi wa habari Mkoa wa Arusha,Claud Gwandu alimpongeza
Mdau huyo kwa msaada wake huo na kuwataka wadau wengine kujitokeza
kusaidia kada hiyo
Alimshukuru Mdau huyo
kuikumbuka kada hiyo na kuona umuhimu wao wa kuwapatia vitendea kazi
hivyo kipindi hichi cha janga la Corona ambavyo vitawafanya kufanya kazi
zao wakati huu wa janga la Ugonjwa wa Covid 19.
No comments :
Post a Comment