Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na
Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa wizara, jijini
Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa(Nida) wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi
wanaofika kuomba vitambulisho.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dkt. Anold Kihaule (kulia)
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi
wa wizara, jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji
wasiotoa huduma stahiki kwa wananchi wanaofika kuomba vitambulisho
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, George Simbachawene akijibu maswali ya Waandishi wa
Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi
wa wizara, jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuwashughulikia watendaji wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) wasiotoa huduma stahiki kwa
wananchi wanaofika kuomba vitambulisho.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu,Dodoma
………………………………………………………………………………………….
Serikali imesema
mashine chakavu ndio chanzo cha ucheleweshaji wa vitambulisho vya NIDA
kwa wananchi wake hapa nchini, na badala yake wamenunua mashine mpya
yenye thamani ya sh bilion 8.5 yenye uwezo wa kufyatua vitambulisho 9000
kwa saa.
Mpaka sasa tayari
NIDA imefanikiwa kutoa vitambulisho milioni sita na kutambua wananchi
milioni 21. 8, hadi sasa kati ya watu 27. 7 waliotarajiwa kusajiliwa.
Jumla ya namba za kipekee za utambulisho ni milioni 17. 8 zilikiwa zimezalishwa na zinaweza kutumika katika utambuzi wa watu.
Akizungumza na
waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene
alisema tayari serikali imenunua mashine mpya ambazo zitakamilishwa
kufungwa April mwaka huu kwa ajili ya kuanza kufanya kazi.
Alisema mtambo huo
mpya una uwezo wa kuzalisha vitambulisho 9, 000 kwa saa jambo ambalo kwa
siku nzima wanauwezo wa kutoa vitambulisho vya kutosha kwa wananchi
wake.
Alisema mitambo mipya
na ikishirikiana na ile ya zamani wanaamini watatoa vitambulisho vingi
ambapo wanatarajia kukamikisha zoezi hilo ndani ya miaka miwili.
“Safarii hii
vitambulisho vitakuwa bora awali vilivyotolewa havikuwa na ubora
kutokana na mashine kuwa chakavu, ” alisema Simbachawene.
Alisema awali mtambo
ulikiwa ukizalisha vitambulisho 500 lakini hivi sass vitaboreshwa na
kuzalishwa vitambulisho vingi kwa siku ili kukamilisha zoezi hilo.
Hata hivyo aliwaomba
radhi wananchi kutokana na kupata shida katika zoezi hilo hivyo
amewaahidi hivi sasa litafanyika kwa haraka zaidi.
Alisema mashine hizo
ni bora na zitafanikiwa kukamikisha zoezi hilo ndani ya miaka miwili
kwa watanzania wote au pungufu ya miaka hiyo.
Alisema serikali
ilivyojipanga kutekeleza zoezi hilo mamlaka imeendelea na ukamilishaji
wa ufungaji mashine wa mitambo ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha
vitambulisho 9, 000 kwa saa moja na zoezi la uzalishaji vitambulisho
litaanza mwishoni mwa Aprili.
Nida kwa kushirikiana
na Idara ya Uhamiaji Kamati za Ulinzi na usalama Idara ya wakimbizi na
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.
Waziri Simbachawene alisema kutokana na utendaji usioridhisha wanatarajia kufanya mabadiliko ndani ya NIDA ili kuboresha.
Alisema pia watakuwa makini katika ugawaji wa vitambulisho kwa wageni wakaazi na wakimbizi.
Zoezi la utoaji
vitambulisho litaendelea ambapo hadi sasa ni watu milioni sita pekee
ndio wamekabidhiwa vitambulisho vya taifa kati ya milioni 27. 7
waliotarajiwa kusajiliwa
No comments :
Post a Comment